Rogasyani wa Karthago

Rogasyani wa Karthago (kwa Kilatini: Rogatianus; 256 hivi) alikuwa padri wa Karthago (leo nchini Tunisia) ambaye aliachiwa na askofu Sipriani mfiadini jukumu la kusimamia jimbo wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.

Baadaye aliteswa na kufungwa kwa imani yake pamoja na Felichisimi[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Oktoba[2][3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.