Salutaris Melchior Libena

Salutaris Melchior Libena ni Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Ifakara, katika mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania.

Alizaliwa huko Itete tarehe 23 Novemba 1963 na baada ya masomo ya ngazi mbalimbali alipewa upadrisho katika Jimbo Katoliki la Mahenge tarehe 29 Juni 1991.

Tarehe 28 Januari 2010 aliteuliwa na Papa Benedikto XVI kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam kwa jina la jimbo la zamani la Sutunurca, akapewa daraja takatifu ya uaskofu na Kardinali Polikarp Pengo tarehe 19 Machi 2010.

Tarehe 14 Januari 2012 aliteuliwa na Papa huyohuyo kuchunga jimbo jipya la Ifakara, ambamo yeye ni mwenyeji, akiwa askofu wa kwanza kutoka kabila la Wandamba.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.