Sanctius wa Lyon ni mmojawapo kati ya wafiadini wa Lyon wanaoheshimiwa kama watakatifu[1].

Ni kwamba mwaka 177 dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo ilisababisha mauaji makubwa katika mji mkuu wa Gallia, jina lake Lyon.

Kati yao, ni maarufu hasa askofu Potinus wa Lyon na bikira Blandina wa Lyon. Wengine ni huyo Sanctius, shemasi, halafu Alexander wa Lyon.Attalus wa Lyon, Espagathus wa Lyon, Maturus wa Lyon, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, JeminianI, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia. Baadhi walifia gerezani, baadhi waliuawa katika kiwanja cha michezo mbele ya maelfu ya watazamaji, ama kwa kwa kukatwa kichwa ama kwa kutupwa waliwe na wanyamapori.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.