Attalus wa Lyon, mwenye asili ya Pergamo, leo nchini Uturuki, ni mmojawapo kati ya wafiadini wa Lyon wanaoheshimiwa kama watakatifu [1].

Ni kwamba mwaka 177 dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo ilisababisha mauaji makubwa katika mji mkuu wa Gallia, jina lake Lugdunum (siku hizi Lyon).

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Juni[2], pamoja na wenzake 47: askofu Potinus wa Lyon na mtumwa bikira Blandina wa Lyon, Aleksanda, Vezi Espagati, Maturus, shemasi Sanctius, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, JeminianI, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia. Baadhi walifia gerezani, baadhi waliuawa katika kiwanja cha michezo mbele ya maelfu ya watazamaji, ama kwa kwa kukatwa kichwa ama kwa kutupwa waliwe na wanyamapori.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.