Shebeli
Shebeli (pia: Shabelle, Scebelli, Shabell, Shebele) ni tawimto la mto Juba linalobeba maji yake kutoka nyanda za juu za Ethiopia kuelekea Bahari ya Uhindi ingawa mara nyingi inakauka katika jangwa la Somalia kabla ya kufikia mdomo wake.
Chanzo cha Shebeli kiko katika milima ya Batu (Ethiopia) takriban km 200 kusini kwa Addis Ababa.
Baada ya mwendo wa km 920 mto unaingia Somalia ikielekea Mogadishu. Karibu na mji unageukia kusini-magharibi na kufuata mstari wa pwani ya Bahari Hindi kwa umbali wa km 20-40 ndani ya bara.
Baada ya mwendo wa km 900 ndani ya Somalia lalio lake linaingia katika mto Juba lakini baada ya Mogadishu Shebeli ni kavu kwa sehemu kubwa ya mwaka.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- en: Map of the Shebelle River basin at Water Resources eAtlas Ilihifadhiwa 24 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- en: Hydropolitics in the Horn of Africa Ilihifadhiwa 26 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- en: "Ethiopia: Rains pound Somali region as death toll rises", IRIN, 5 Mei 2005
- en: "Floods plague Horn of Africa, wash away refugee shelters" - UN News
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Shebeli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |