Uhuru wa Tanganyika
Uhuru wa Tanganyika ulipatikana tarehe 9 Desemba 1961.
Eneo la Tanganyika, ambalo awali, pamoja na Rwanda na Burundi, liliunda koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, lilikuwa linasimamiwa na Uingereza kuanzia mwaka 1916 mpaka 1961.
Kwanza lilikuwa linasimamiwa chini ya utawala wa kijeshi.
Kuanzia tarehe 20 Julai 1922, lilirasimishwa kuwa ndani ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa chini ya utawala wa Waingereza.
Kuanzia mwaka 1946, liliongozwa na Uingereza kama eneo la kudhaminiwa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa hadi siku ya kupata uhuru.
Mhusika mkuu wa uhuru huo alikuwa Julius K. Nyerere pamoja na chama cha TANU.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uhuru wa Tanganyika kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |