Siku ya Kiswahili Duniani
(Elekezwa kutoka Siku ya Lugha ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa)
Siku ya Kiswahili Duniani (kwa Kiing. World Kiswahili Language Day) ni tarehe 7 Julai iliyoteuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuadhimisha lugha ya Kiswahili kila mwaka kuanzia 2022[1].
Mkutano Mkuu wa UNESCO uliamua kwenye tarehe 23 Novemba 2021 kutangaza Siku ya Kiswahili Duniani iadhimishwe kila mwaka.
Kwa azimio hilo UNESCO inalenga kutambua kuwa
- Kiswahili ni kati ya lugha za Kiafrika zinazotumiwa zaidi, pia ni lugha ya Kiafrika inayotumiwa zaidi katika Afrika kusini mwa Sahara. Kipo kati ya lugha 10 zinazotumiwa na wasemaji wengi duniani.
- Ni lugha ya mawasiliano (lingua franca) katika nchi nyingi za Afrika ya Kati na Afrika ya Kusini pamoja na Mashariki ya Kati. Inafundishwa katika vyuo vingi kote duniani.
- Ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Tarehe 7 Julai ilichaguliwa kukumbuka:
- 7 Julai 1954 ambako chama cha TANU chini ya uongozi wa Julius Nyerere kiliamua kutumia Kiswahili kwa ajili ya shughuli zake za kulenga uhuru wa Tanganyika
- 7 Julai 2000 ambako mkataba juu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki iliyofufuliwa ulipata kuwa rasmi. Jumuiya hiyo iliunganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zenye wasemaji wengi wa Kiswahili.
Washairi mashuhuri wa Kiswahili
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- WORLD KISWAHILI LANGUAGE DAY, azimio la Mkutano Mkuu wa UNESCO wa 23 Novemba 2021, tovuti ya UNESCO Digital Library, iliangaliwa Julai 2022
- Kiswahili Language Day 2022, tovuti ya UNESCO