Simeoni bar Sabas na wenzake

Simeoni bar Sabas na wenzake zaidi ya 100, wakiwemo maaskofu, mapadri na watawa (walifariki nchini Uajemi, 345) walikuwa Wakristo waliofungwa muda mrefu wakauawa kwa sababu ya kukataa kumkana Yesu Kristo na kuabudu jua katika dhuluma ya mfalme Sabor II [1][2].Kati yao wanatajwa kwa jina mapadri Abdhaykla na Anania, pia afisa Pusayk.

Picha takatifu ya Mt. Simeoni katika mavazi ya ibada.

Baada ya wengine wote kukatwa shingo kwa upanga mbele ya Simeoni, askofu mkuu wa Seleukia-Ktesifon, leo Al-Mada'in nchini Iraki, kuanzia mwaka 324, aliyekuwa anawatia moyo, wa mwisho mwenyewe alikatwa kichwa.

Tangu kale wanaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Aprili[3] au 30 Aprili au 17 Agosti.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92746
  2. A near-contemporary 5th century Christian work, the Ecclesiastical History of Sozomen, contains considerable detail on the Persian Christians martyred under Shapur II. Sozomen estimates the total number of Christians killed as follows: The number of men and women whose names have been ascertained, and who were martyred at this period, has been computed to be upwards of sixteen thousand, while the multitude of martyrs whose names are unknown was so great that the Persians, the Syrians, and the inhabitants of Edessa, have failed in all their efforts to compute the number. — Sozomen, in his Ecclesiastical History, Book II, Chapter XIV
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.