Simoni wa Rojas
Simoni wa Rojas (Valladolid, Hispania, 28 Oktoba 1552 - Madrid, 29 Septemba 1624) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Watrinitari, yaani watawa wa Utatu mtakatifu, waliojitoa kabisa kwa ajili ya kukomboa Wakristo waliotekwa utumwani.
Ingawa kwa miaka mingi alitakiwa kuongozana na malkia na kuishi kati ya fahari za ikulu, alizidi kuishi kwa unyenyekevu na ufukara, akikataa daima vyombo vya usafiri na malipo. Alikuwa na huruma kubwa kwa maskini, ari katika ibada kwa Mungu na heshima ya pekee kwa Bikira Maria [1].
Alitangazwa na Papa Klementi XIII kuwa mwenyeheri tarehe 19 Machi 1766, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 3 Julai 1988.
Sikukuu yake ni tarehe 28 Septemba[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Matthew Bunson, Margaret Bunson, Our Sunday Visitor's Encyclopedia of Saints, Our Sunday Visitor Publishing, p 757.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |