Sopa ni kata ya Wilaya ya Kalambo katika Mkoa wa Rukwa, Tanzania. Kata hii iliwahi kuwa sehemu ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini ikahamishwa kwenye wilaya mpya ya Kalambo mwaka 2012.

Kata ya Sopa
Nchi Tanzania
Mkoa Rukwa
Wilaya Kalambo
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 13,222

Kata ya Sopa ina jumla ya vijiji saba: Sopa, Mtuntumbe, Kasitu, Tatanda, Ilambila, Kalaela na Kamawe.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 13,222 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,320 waishio humo.[2]

Utamaduni wa wakazi wa kata ya Sopa ni ule wa Wafipa wanaotumia lugha ya Kifipa katika mawasiliano.

Kuna jumla ya sekondari 2, ikiwemo Ulungu inayopatikana kijiji cha Tatanda, pia shule ya sekondari Kanyele inayopatikana kijiji cha Sopa.

Historia hariri

Sopa ni neno lililotokana na njia, njia ambayo Wajerumani walikuwa wakiitumia katika misafara yao; njia ilikuwa ikikatisha pembezoni mwa kijiji, ikitokea Lusaka, kupita Tatanda na kukatisha Sopa kuelekea Kasanga.

Njia hiyo iliweza kutumiwa na wakazi tofauti, awali ya yote kijiji kiliitwa Sote, baada ya kuzoeleka na wakazi au Wajerumani ndipo kijiji kikaitwa Sopa.

Kijiji hicho kilitawaliwa na viongozi tofauti akiwemo Alfredy Mwanga Sokoni.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Kalambo - Mkoa wa Rukwa - Tanzania  

Kanyezi | Kasanga | Katazi | Katete | Kilesha | Kisumba | Legezamwendo | Lyowa | Mambwekenya | Mambwe Nkoswe | Matai | Mbuluma | Mkali | Mkowe | Mnamba | Mpombwe | Msanzi | Mwazye | Mwimbi | Samazi | Sopa | Sundu | Ulumi

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sopa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.