Sotere wa Roma (alifariki mjini Roma, Italia, 304) alikuwa bikira wa ukoo maarufu aliyeuawa kwa sababu alikataa kutoa sadaka kwa miungu kutokana na imani yake ya Kikristo.

Kwa sababu hiyo alitukanwa na kuteswa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo akauawa kwa upanga wakati wa kaisari Dioklesyano.

Habari zake zimesimuliwa na Ambrosi ambaye alikuwa na undugu naye[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 11 Februari[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.