Spiridoni wa Tremetusia

Spiridoni wa Tremetusia (kwa Kigiriki: Ἅγιος Σπυρίδων; Askeia, Kupro, 270 hivi – Tremetusia 348) alikuwa askofu wa mji huo wa Kupro.

Picha takatifu ya Mt. Spiridoni.
Picha takatifu ikimuonyesha Mt. Spiridoni (katikati, mbele) akimnyamazisha Ario (kulia, akizuia mdomo kwa mkono) wakati wa mtaguso wa kwanza wa Nisea.
Mchoro wa ukutani wa Mt. Spiridoni katika Zemen Monastery, Bulgaria.

Tangu kale anaheshimiwa na Ukristo wa Mashariki na Ukristo wa Magharibi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa mashariki tarehe 25 Desemba na magharibi tarehe 12 Desemba[1].

Maisha hariri

Alipokuwa mchungaji alianza kujulikana kwa maisha yake ya kiroho. Alioa na kuzaa binti mmoja, Irene.

Alipofiwa mke wake, Spiridoni aliingia katika monasteri, na binti yake vilevile.

Hatimaye Spiridoni akawa askofu wa Tremetusia, katika wilaya ya Larnaca. Alishiriki mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325), aliposaidia sana kupinga teolojia ya akina Ario.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.