Sydney Anne Bristow (amezaliwa tar. 17 Aprili 1975) ni jina la kutaja muhusika mkuu katika mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Alias. Uhusika umechezwa na Jennifer Garner. Yeye ni mwanamke wa Kimarekani mwenye asili ya Kirusi-Kimarekani ambaye anafanya kazi kama mpelelezi wa CIA.

Sydney Bristow
muhusika wa Alias
Mwonekano wa kwanza "Truth Be Told"
(sehemu ya 1.01)
Mwonekano wa mwisho "All the Time in the World"
(sehemu 5.17)
Imechezwa na Jennifer Garner
Maelezo
Majina mengine Bluebird
Freelancer
Mountaineer
Phoenix
Jinsia Kike
Kazi yake Kachero ugani wa SD-6
CIA
The Covenant muuaji
(DSR kachero mara mbilit)
APO kachero ugani
Taji Agent Sydney Bristow
Ndoa Michael Vaughn
(mume)
Significant other(s) Danny Hecht
(fiancé; deceased)
Watoto Isabelle Vaughn
(binti, amezaa na Michael)
Jack Vaughn
(mtoto wa kiume, amezaa na Michael)
Ndugu Jack Bristow
(baba; amefariki)
Irina Derevko
(mama; amefariki)
Elena Derevko
(mama mdogo; amefariki)
Katya Derevko
(mama mdogo)
Nadia Santos
(dada wa kufikia; amefariki)
Utaifa Mmarekani

Sydney anaonekana katika mfululizo akiwa mama mshupavu kimuonekano na hata kihisia halkadhalika. Amekuwa akijishughulisha na baadhi ya kazi za viwewe vya maana kwa miaka zaidi: kifo cha mchumba wake, kifo cha rafiki yake wa karibu, kugundua kwake kwamba mama yake alikuwa mpelelezi wa zamani wa KGB, utenganisho wake na marafiki zake waliowengi na uwastani wa kazi yake na mabadiliko ambayo hana budi kuyavumilia kuwa mpelelezi na kuishi katika hali ya kawaida. Sydney ana maarifa ya hali ya juu katika Krav Maga na ni hodari sana wa malugha, anazungumza Kiingereza, Kirusi, Kijerumani, Kigiriki, Kiholanzi, Kifaransa, Kiitalia, Kihispania, Kireno, Kinorwei, Kiswidi, Kiromania, Kihungaria, Kiyahudi, Kiubzbeki, Kiarabu, Kiajemi, Kiurdu, Kiindonesia, Kikantonese, Kimandarini, Kijapani, Kikorea, Kihindi, Kivietnamu, Kipolandi, Kiserbia, Kicheki, Kiukraini, na Kibulgaria katika vipengele mbalimbali vya mfululizo. Katika mfulizo majina msimbo anayotumia ni pamoja na Bluebird, Freelancer, Mountaineer, na Phoenix.

Maelezo ya kiuwasifu

hariri

Sydney Bristow alizaliwa kunako mwezi wa 17 Aprili 1975. Kwa miaka yake sita ya kwanza aliishi maisha yake na wazizi wake wote wawili, Jack na Laura Bristow (jina halisi ni Irina Derevko). Ijapokuwa kazi ya baba'ke na kina CIA ilimweka mbali na famili yake kwa mara kadhaa. Sydney na familia yake walikuwa wakiishi katika kijiji cha Maryland hadi hapo, akiwa na umri wa miaka miwili, Jack akahamishwa huko mjini Los Angeles. Mnamo mwaka wa 1981, mama'ke, ambaye pia alikuwa kachero kanzu wa KGB, amebandisha kifo chake ili kuzuia kina FBI wasimtie nguvuni.

Baada ya hapo Jack alitiwa mbaroni kwa muda fulani, kwa sababu iliamianika kwamba pia alikUwa mmoja kati ya wala-njama wakubwa. Jack amemvika Arvin Sloane akiwa kama mlinzi wa Sydney wa muda. Sydney akaenda kuishi na Sloane na mke wake Emily, kwa muda (Tambua kwamba hii ilikuwa kinyumenyume kama jinsi ilivyoelezwa awali kwamba Sydney hajaonana na Arvin wala Emily hadi hapo Sydney alipoanza kufanya kazi katika SD-6. Ingawa Sydney alieleza kwamba alikuwa na pengo kubwa la kumbukumbu katika kipindi cha kifo cha mama yake kinaashiria kwamba huenda ikawa kuna jambo lingine lilitokea na kuondoa kumbukumbu zake za kipindi hicho).

Wakati Jack alivyomalizana na zahama lake, akaanza ulevi wa kupitiliza na kuwa baba asiyeonekana zaidi, ana-mwacha Sydney akielelewa na mfanyakazi wa ndani. Katika maisha yake ya utoto ya baadaye, Sydney akaanza kuonesha uwezo wa kukabiliana na kutatua matatizo kadha wa kadha wakati yupo shule.

Alivyofikisha miaka 19, huku akiwa mpya chuoni, mtu mmoja alimsogelea na kumwambia kwamba anafanya kazi na CIA na hivyo basi wanataka kumfanyia majaribio kama ataweza kufitisha hali yake ya kuwa kachero hai wa CIA. Awalia alikataa, lakini baadaye alikubali kujiunga nao. Baada ya kukutana na jumuia aliamini walikuwa kina Central Intelligence Agency, amesaidia "madazeni ya mikataba isiyotakiwa-kuonekana na wengine" na kumpatia kazi.

Wamempatia Sydney kazi akiwa kama afisa msaidizi katika ghorofa ya ishirini ya benki, benki ya ushirika iliyopo mjini Los Angeles. Aliamini kwamba benki ilikuwa inahusiana kiasi fulani na kina CIA. Alipomwambia baba'ke kuhusus kazi yake baada ya mwezi, amemtaka aache kwa sababu akiwa kama kachero mara-mbili ndani ya SD-6, alifahamu fika kama benki ilikuwa kwa mbele. Sydney alikataa kwa hasira kuacha na hii imepelekea mwanzo wa utengano wa mahusiano yao.

Hatimaye akaambiwa yupo tayari kwa uhamisho, ambapo ilihusisha miezi minane ya mafunzo. Ilikuwa kipindi cha mafunzo kwa Sydney kusikia istilahi ya SD-6. Kwa kipindi hiki, aliamini kwamba SD-6 ilikuwa inahusiana na kina CIA, kwamba kilikuwa kitengo kinachoendesha operesheni zake kwa siri cha CIA, kinapewa pesa na kina CIA katika bajeti zao za siri. Operesheni hii ni ya siri kwa kiasi kikubwa sana, inafichwa hata kwa wazee wa baraza. Wamemfanya aamini kwamba SD-6 ilikuwa moja kati ya vitengo ambavyo havitakiwi vijiendeshe kupitia Langley, Virginia.

Marejeo

hariri