Tanzania Breweries Limited

Tanzania Breweries Ltd ni kampuni nchini Tanzania inayohusika katika uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa bia, pombe mbalimbali na vinywaji visivyo na kilevi nchini Tanzania.

Tanzania Breweries Limited
Makao MakuuBuguruni, Dar es Salaam, Tanzania
Mapatoincrease bilioni TSh 176 (March 2013)
Total equityincrease bilioni TSh487 (March 2013)[1]
MmilikiAB InBev

Makao makuu ya TBL yapo . Kampuni inaendesha viwanda vinne Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. [2]

TBL imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam. Mmiliki wa kampuni ni SABMiller wa Afrika Kusini.

Historia

hariri

1930 - 1959

hariri

Kampuni hiyo ilianzishwa mnamo 1933 kwa jina la Tanganyika Breweries wakati wa ukoloni wa Kiingereza. Ikanunuliwa kampuni ya Kenya Breweries Limited (KBL, Nairobi) mnamo 1935. Tangu 1936, makampuni yote mawili yaliunganishwa kuwa East African Breweries Limited (EABL).

1960 - 1989

hariri

Mnamo mwaka wa 1964, jina la kampuni upande wa Tanzania lilibadilishwa kutoka kuwa Tanzania Breweries Limited kufuatia maungano wa kisiasa wa Tanganyika na Zanzibar.

Mwaka 1967 Serikali ya Tanzania ilianza kuekeza hapa ikanunua asilimia 45 za hisa. Baadaye serikali iliendelea kutaifisha kampuni yote na kuiendesha kama kampuni ya umma kulingana na msimamo wa Azimio la Arusha . [3] Baada ya kutaifishwa mnamo 1967, TBL ilisimamiwa vibaya ikaendelea kuleta hasara kibiashara; ubora wa bia zake ulishuka pia ilishindwa kutengeneza bidhaa za kutosheleza soko la nchi.

1990 - 1999

hariri

Mnamo 1993 serikali ya Tanzania iliingia katika ubia na ushirikiano na South African Breweries International (sasa SABMiller) iliyokabidhiwa utawala wa TBL. SABl waliwekeza dolar za Kimarekani milioni 22.5 katika TBL na kupata hivyo kumiliki asiimia 50 za TBL. Utawala wa SABMiller ulifaulu kuondoa hitilafu ya awali na kuongeza uzalishaji wa bia mara tatu katika kipindi cha miaka mitatu iliyofuata. [4]

Kwenye Septemba 1998 TBL iliorodheshwa tena kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

2000 - 2009

hariri

Mnamo 2002, EABL ya Kenya ilinunua asilimia 20 za hisa za TBL, na kusaini mikataba ya leseni na kampuni ya SABl ya Afrika Kusini. Pande mbili zilipatana kugawa soko la Afrika ya Mashariki kati yao; EABL ilikabidhi kiwanda cha bia cha Kibo kwa TBL, na SABl iliondoka katika soko la Kenya. Kufuatana na mapatano haya TBL ilishika asilimia 98% za soko la bia nchini Tanzania ifikapo mwaka 2004. [5]

Tangu mwaka 2010

hariri

Mnamo mwaka wa 2010, EABL iliiliondoka katika makubaliano haya na TBL, ikauza hisa zake na kununua hisa za asilimia 51 katika Serengeti Breweries, ambayo ni mtengenezaji wa bia mkubwa wa pili nchini Tanzania. [6]

Mnamo Machi 2013, TBL ilinunua asilimia 60 za hisa za Darbrew Limited kwa TShs 8,816 Milioni na kupata udhibiti wa kampuni hiyo inayopika pombe za kienyeji. [5]

Mnamo Machi 31, 2013, TBL ilishika asilimia 74 za soko la vinywaji vya pombe nchini Tanzania. Iliuza viwango vikubwa vya bia nje kwa Nile Breweries Limited ya Uganda, Crown Beverage Limited ya Kenya na Zambia Breweries Limited ya Zambia, ambazo zote zinamilikiwa na SABMiller . [5]

 
Chupa ya Kilimanjaro Lager

Mwaka 2016 SABMiller ilinunuliwa na kampuni la Marekani AB InBev (Anheuser-Busch InBev SA/NV)[7].

Makampuni yaliyo chini ya TBL

hariri

Kampuni yaliyo chini ya Tanzania Breweries Limited ni pamoja na: [5]

  1. Tanzania Breweries Limited - Inajihusisha na uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa bia ya kimea, vinywaji vya kimea visivyo vya pombe na vinywaji vya pombe la matunda.
  2. Kibo Breweries Limited - (inamilikiwa kwa %100) inasimamia mali kama mitambo, injini, magari na fenicha kwa makampuni yote ya kundi la TBL
  3. Tanzania Distilleries Limited - (inamilikiwa kwa %65) - inazalisha pombe kali
  4. Darbrew Limited - (inamilikiwa kwa %60) - inazalisha pombe zinazotengenezwa kwa namna ya kienyeji
  5. Mountainside Farms Limited - (%4 za hisa) - inalima shayiri

Bidhaa

hariri

Kwa sasa TBL inauza aina 11 za vinywaji zikiwa pamoja na:

  1. Castle Lager
  2. Castle Lite
  3. Kilimanjaro Lager
  4. Eagle
  5. Balimi
  6. Ndovu Special Malt
  7. Safari Lager
  8. CAstle Milk Stout
  9. Grand Malta
  10. Bia Bingwa
  11. Safari Sparkling Water

Umiliki

hariri

Hisa za Tanzania Breweries Limited zinauzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, chini ya kifupi: TBL .

Kufuatana na taarifa ya mwaka 2018 jumla ya hisa 295,056,063 za kampuni zilimilikiwa na wafuatao [8]:

Wanahisa wa Tanzania Breweries Limited
Cheo Jina la Mmiliki Umiliki wa Asilimia
1 AB-InBev Africa BV (zamani SABMiller Africa BV) 63,95
2 Wanahisa wengine wa nje ya Tanzania 20,86
3 Wanahisa wa binafsi nchini Tanzania 6,72
4 Mfuko wa Mafao ya Shirika za Umma (PFF) 4.2
5 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) 1.65
6 Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (Unit Trust of Tanzania UTT) 1.44
7 Akiba ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) 0.95
8 Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) 0.24
Jumla 100.00

Utawala

hariri

Tanzania Breweries Limited inasimamiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya watu kumi na Cleopa Msuya anayehudumu kama Mwenyekiti wa kikundi hicho na Philip Redman kama Mkurugenzi Mkuu. [9]

Marejeo

hariri
  1. "Tanzania Breweries Limited Headline Results - March 31, 2013" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-08-25. Iliwekwa mnamo 2020-03-06.
  2. "Commercial Credit Report for Tanzania Breweries Limited - Report Preview". www.crmz.com. Iliwekwa mnamo 2017-09-04.
  3. "History of TBL", SaaHiiHii. (lt) 
  4. (www.e-afacere.ro), E-afacere. "UrsusBreweries". ursus-breweries.ro. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-04. Iliwekwa mnamo 2017-09-04.
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 Tanzania Breweries Limited 2012/13 Annual Report
  6. "EABL gets nod to sell stake in SABMiller's unit". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-02. Iliwekwa mnamo 2020-03-06. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  7. Brown, Lisa. "A-B InBev finalizes $100B billion acquisition of SABMiller, creating world's largest beer company", 11 October 2016. 
  8. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2021-10-16. Iliwekwa mnamo 2020-03-06.
  9. Company Overview of Tanzania Breweries Limited - Board Members

Viungo vya nje

hariri