Tashdidi
Katika fonetiki na fonolojia, tashdidi au kurefusha konsonanti, ni utamkaji wa konsonanti kwa muda mrefu zaidi kuliko ule wa konsonanti moja. [1] Ni tofauti na mkazo. Tashdidi huwakilishwa katika mifumo mingi ya uandishi kwa herufi pacha na mara nyingi huchukuliwa kuwa ni marudufu ya konsonanti. [2] Baadhi ya nadharia za kifonolojia hutumia 'kuongezeka maradufu' kama kisawe cha tashdidi, wakati nyingine zinaelezea matukio mawili tofauti. [2]
Urefu wa konsonanti ni kipengele bainifu katika lugha kadhaa, kama vile Kiarabu, Kiberber, Kideni , Kiestonia, Kifini, Kihindi, Kihungaria, Kiitalia, Kijapani, Kikannada, Kimalayalam, Kipunjabi, Kipolandi na Kituruki.
Tashdidi ya konsonanti na urefu wa irabu hujitegemea katika lugha kama Kiarabu, Kijapani, Kifini na Kiestonia; lakini katika lugha kama Kiitalia, Kinorwei na Kiswidi, urefu wa irabu na urefu wa konsonanti hutegemeana. Kwa mfano, katika Kinorwei na Kiswidi, konsonanti yenye tashdidi hutanguliwa na irabu fupi, huku konsonanti ambayo haina tashdidi hutanguliwa na irabu ndefu. Mfano ni katika maneno ya Kinorwei tak [ tɑːk ] ('dari au paa' la jengo), na takk [ tɑkː ] ('asante').
Fonolojia
haririTashdidi ya konsonanti hubainika katika baadhi ya lugha na kisha huathiriwa na vikwazo mbalimbali vya kifonolojia vinavyotegemea lugha husika.
Katika baadhi ya lugha, kama vile Kiitalia, Kiswidi, Kifaroe, Kiaislandi, na Kiganda, urefu wa konsonanti na urefu wa irabu hutegemeana. Irabu fupi katika silabi iliyosisitizwa karibu kila mara hutangulia konsonanti ndefu au msongamano wa konsonanti, na irabu ndefu lazima ifuatwe na konsonanti fupi.
Katika lugha zingine, kama vile Kifini, urefu wa konsonanti na urefu wa irabu hazitegemeani. Mfano; taka /taka/ 'nyuma', takka /takːa/ 'mekoni' na taakka /taːkːa/ 'mzigo' ni maneno tofauti, yasiyohusiana. Urefu wa konsonanti za Kifini pia huathiriwa na upangaji wa konsonanti.
Katika baadhi ya maneno ambatani ya Kifini, ikiwa neno la awali linaishia kwa e , konsonanti ya awali ya neno lifuatalo litakuwa na tahsdidi: jätesäkki 'mfuko wa takataka' [jætesːækːi] , tervetuloa 'karibu' [terʋetːuloa]. Katika hali kadhaa, v baada ya u inapewa tashdidi na watu wengi: ruuvi 'screw' /ruːʋːi/ , vauva 'mtoto' [ʋauʋːa]. Katika lahaja ya Tampere, ikiwa neno linapokea tashdidi ya v baada ya u , u mara nyingi hufutwa ( ruuvi [ruʋːi] , vauva [ʋaʋːa]), na kwa mfano, lauantai 'Jumamosi', inapokea v [lauʋantai], ambayo inaweza kusababisha kufutwa kwa u ( [laʋːantai]).
Urefu bainifu wa konsonanti kwa kawaida huwekwa kwa konsonanti fulani pekee. Kuna lugha chache sana ambazo zina urefu wa konsonanti za mwanzo/awali; miongoni mwao ni Kimalay cha Pattani, Kichuuk, Kiarabu cha Moroko, lugha chache za Kirumi kama vile Kisisili na Kinapoli pamoja na lahaja nyingi za Kijerumani cha juu cha Kialemani, na ile ya jimbo la Thurgau nchini Uswisi. Baadhi ya Lugha za Afrika, kama vile Kitswana na Kiganda, pia zina urefu wa konsonanti za mwanzo: ni kawaida sana katika Kiganda na huonyesha sifa fulani kisarufi. Katika Kifini cha mazungumzo na Kiitalia, konsonanti ndefu hutokea katika hali maalum.
Mifano
haririLugha za Kiafrika-Kiasia
haririKiarabu
haririKiarabu kilichoandikwa kinaonyesha tashdidi kwa alama ( ḥaraka ) yenye umbo la herufi ndogo ya Kilatini w, inayoitwa شَدَّة shadda : ّ . Inandikwa juu ya konsonanti inayotakiwa kuwa na tashdidi. Shadda mara nyingi hutumika kutofautisha maneno ambayo hutofautiana tu katika urudufu wa konsonanti ambapo neno lililokusudiwa halieleweki wazi kutokana na muktadha. Kwa mfano, katika Kiarabu, vitenzi vya umbo la kwanza na vitenzi vya umbo la pili hutofautiana tu katika urudufu wa konsonanti ya kati ya mzizi wa utatu katika umbo la mwisho. Mfano, درس darasa (lenye alama kamili: دَرَسَ) ni kitenzi cha umbo la kwanza chenye maana ya kusoma, ambapo درّس darrasa (lenye alama kamili: دَرَّسَ) ni kitenzi cha umbo la pili kinacholingana, chenye konsonanti r ya kati, kupewa maradufu kumaanisha kufundisha .
Kitamzighi
haririKatika Kitamazighi, kila konsonanti ina mwenza wake wa tashdidi, na tashdidi huleta tofauti kimsamiati. Tofauti kati ya konsonanti ya pekee na ya tashdidi inathibitishwa katika nafasi ya kati ya neno na vile vile katika nafasi za mwanzo na za mwisho.
- ini 'sema'
- inni 'ambao'
- akal 'ardhi, udongo'
- akkal 'hasara'
- imi 'mdomo'
- immi 'mama'
- ifis 'fisi'
- ifiss 'alikuwa kimya'
- tamda 'dimbwi, ziwa'
- tamedda 'shakivale, kipanga'
Lugha za Kiaustronesia
haririLugha za Kiaustronesia nchini Ufilipino, Mikronesia na Sulawesi zinajulikana kuwa na konsonanti zenye tashdidi [3]
Kikavalani
haririLugha ya Kiformosane Kikavalani hutumia tashdidi kuashiria ukubwa, kama ilivyo kwa sukaw 'mbaya' dhidi ya sukkaw 'mbaya sana'. [3]
Lahaja za Kimalei
haririTashdidi ya neno-awali hutokea katika lahaja mbalimbali za Kimalei, hasa zile zinazopatikana katika pwani ya mashariki ya Rasi ya Malei kama vile Kimalei cha Kelantan-Patani na Kimalei cha Terengganu . [4] [5] Tashdidi katika lahaja hizi za Kimalei hutokea kwa madhumuni mbalimbali kama vile:
- Ili kuunda neno fupi au kirai:
- buwi /buwi/ > /wːi/ 'toa'
- ke darat /kə darat/ > /dːarat/ 'kwenda/kwa/kutoka ufukweni'
- Ubadilishaji wa urudufishaji kwa matumizi yake mbalimbali (kama kuashiria wingi, kuunda neno tofauti, n.k.) katika Kimalei sanifu:
- budak-budak /budak budak/ > /bːudak/ 'watoto'
- layang-layang /lajaŋ lajaŋ/ > /lːajaŋ/ 'kishada
Kituvalu
haririLugha ya Kipolinesia ya Kituvalu huruhusu tashdidi za neno-awali, kama vile mmala 'imepikwa kupita kiasi'. [6]
Lugha za Kihindi-kiulaya
haririKiingereza
haririKatika fonolojia ya Kiingereza, urefu wa konsonanti hautofautishi ndani ya mzizi wa maneno . Kwa mfano, baggage hutamkwa / ˈbæ ɡ ɪ dʒ /, si */bæɡːɪdʒ/. Hata hivyo, tashdidi ya kifonetiki hutokea kwa kiasi kidogo.
Tashdidi hupatikana katika maneno na mofimu wakati konsonanti ya mwisho katika neno fulani na konsonanti ya kwanza katika neno lifuatalo ni sawa frikativo, nazali au infijari. [7]
Kwa mfano:
- b: subbasement [ˌsʌbˈbeɪsmənt]
- d: midday [mɪdˈdeɪ]
- f: life force [ˈlaɪfˈfors]
- g: egg girl [ˈɛɡ.ɡɝl]
- k: bookkeeper [bʊk̚kiː.pə(ɹ)]
- l: guileless [ˈɡaɪl.ləs]
- m: calm man [ˌkɑːmˈmæn] or roommate [ˈrum.meɪt] (katika baadhi ya lahaja) or prime minister [ˌpɻaɪmˈmɪnɪstəɹ]
- n: evenness [ˈiːvənnəs]
- p: lamppost [ˈlæmp̚poʊst] (cf. lamb post, compost)
- r: interregnum [ˌɪntəɹˈɹɛɡnəm] or fire road [ˈfaɪəɹ.ɹoʊd]
- s: misspell [ˌmɪsˈspɛl] or this saddle [ðɪsˈsædəl]
- sh: fish shop [ˈfɪʃ.ʃɒp]
- t: cattail [ˈkæt̚teɪl]
- th: both thighs [boʊθ'θaɪz]
- v: live voter [ˈlaɪv.vəʊtə(ɹ)]
- z: pays zero [peɪzˈziːˈɹo]
Kwenye konsonanti za afrikato, hii haitokei. Kwa mfano:
- orange juice [ˈɒɹɪndʒ.dʒuːs]
Mara nyingi, kutokuwepo kwa urudufu huu haiathiri maana, ingawa inaweza kumchanganya msikilizaji kwa muda. Zifuatazo zinawakilisha mifano ambapo uwepo wa urudufu unaathiri maana katika lafudhi nyingi:
- ten nails versus ten ales
- this sin versus this inn
- five valleys versus five alleys
- his zone versus his own
- mead day versus me-day
- unnamed [ʌnˈneɪmd] versus unaimed [ʌnˈeɪmd]
- forerunner [ˈfɔːɹˌɹənəɹ] versus foreigner [ˈfɔːɹənəɹ] (katika baadhi ya lafudhi za Kiingereza cha Marekani)
Katika baadhi ya lahaja tashdidi pia hupatikana katika baadhi ya maneno wakati kiambishi tamati -ly kinapofuata mzizi unaoishia kwa -l au -ll, kama katika:
- solely [ˈsoʊl.li]
lakini sivyo
- usually [ˈjuːʒ(ʊə)li]
Kifaransa
haririKatika Kifaransa, tashdidi kwa kawaida haihusiki kifonolojia na kwa hivyo hairuhusu maneno kutofautishwa: mara nyingi inalingana na lafudhi ya kusisitiza ( c'est terrifiant nilitambua [ˈtɛʁ.ʁi.fjɑ̃]), au hukutana na vigezo vya urekebishaji mwingi: mtu "husahihisha" matamshi ya mtu, licha ya fonolojia ya kawaida, kuwa karibu na utambuzi ambao mtu hufikiria kuwa sahihi zaidi: kwa hivyo, neno illusion wakati mwingine hutamkwa [il.lyˈzjɔ̃] kwa ushawishi wa tahajia.
Hata hivyo, tashdidi inaleta utofauti katika visa vichache. Kauli kama vile elle a dit ('alisema(ke)') ~ elle l'a dit ('alikisema(ke)') /ɛl a di/ ~ /ɛl l‿a di/ kawaida inaweza kutofautishwa kwa tashdidi. Katika matamshi endelevu zaidi, tashdidi hutofautisha hali ya masharti (na pengine ya wakati ujao) na isiyo kamilifu: courrai 'nitakimbia' /kuʁ.ʁɛ/ /kuʁ.ʁɛ/ dhidi ya courais 'nilikimbia' /ku.ʁɛ/ /ku.ʁɛ/.
Kigiriki
haririKatika Kigiriki cha Kale, urefu wa konsonanti ulikuwa tofauti, kwa mfano, μέλω [mélɔː] 'Nina maslahi' dhidi ya μέλλω [mélːɔː] 'Naenda'. Tofauti imepotea katika Kigiriki cha kisasa na lahaja nyingine nyingi, isipokuwa lahaja ya Kupro, baadhi ya lahaja za kusini mashariki mwa Aegea na Italia.
Kihindustani
haririTashdidi ni kawaida katika Kihindi na Kiurdu. Haitokei baada ya irabu ndefu na hupatikana katika maneno ya asili ya Kiindi na Kiarabu, lakini si katika yale ya asili ya Kiajemi. Katika Kiurdu, tashdidi inawakilishwa na alama ya Shadda, ambayo ni kawaida kuachwa katika maandishi, huwa inaandikwa pale ambapo kuna utata. Katika Kihindi, tashdidi inawakilishwa kwa kufanya urudufu wa konsonanti, iliyoambatanishwa na alama ya Virama .
Unukuzi | Kihindi | Kiurdu | Maana | Etimolojia |
---|---|---|---|---|
pattā | पत्ता | پَتَّہ | 'jani' | Kisanskriti |
abbā | अब्बा | اَبّا | 'baba' | Kiarabu |
dajjal | दज्जाल | دَجّال | 'mpinga kristo' | |
ḍabbā | डब्बा | ڈَبَّہ | 'sanduku' | Kisanskriti |
jannat | जन्नत | جَنَّت | 'mbinguni' | Kiarabu |
gaddā | गद्दा | گَدّا | 'godoro' | Kisanskriti |
Kiitaliano
haririKiitaliano kinajulikana kati ya lugha za Kirumi kwa konsonanti zake nyingi zenye tashdidi. Katika Kiitaliano Sanifu, tashdidi huandikwa kwa konsonanti mbili, na tashdidi huanisha tofauti katika maana. [8] Kwa mfano, bevve, ikimaanisha 'alikunywa', huku beve ('anakunywa'),
Konsonanti mbili au ndefu hutokea si tu ndani ya maneno bali pia katika mipaka ya maneno, na kisha hutamkwa lakini si lazima kuandikwa: chi+ sa = chissà ('nani anajua') [kisˈsa] na vado a casa ('Naenda nyumbani') [ˈvaːdo a kˈkaːsa]. Konsonanti zote isipokuwa /z/ zinaweza kupata tashdidi.
Kilatini
haririKatika Kilatini, urefu wa konsonanti ulileta tofauti, kama katika neno anus 'mzee mwanamke' na annus 'mwaka'. Tashdidi zilizorithiwa kutoka Kilatini bado zipo katika Kiitaliano, ambapo [ˈanno] anno na [ˈaːno] ano zatofautiana /nn/ na /n/ kama katika Kilatini. Imekaribia kupotea kabisa katika Kifaransa na imepotea kabisa katika Kiromania.
Kinepali
haririKatika Kinepali, konsonanti zote zina konsonanti za tashdidi isipokuwa /w, j, ɦ/. Tashdidi hutokea tu kati ya neno. [9] Mifano:
- समान – 'equal' [sʌmän]; सम्मान [sʌmːän] – 'heshima'
- सता – 'disturb!' [sʌt̪ä]; सत्ता [sʌt̪ːä] – 'mamlaka'
- पका – 'cook!' [pʌkä]; पक्का [pʌkːä] – 'yakini'
Kinorwe
haririKatika Kinorwe, tashdidi inaonyeshwa kwa maandishi na konsonanti mbili. Tashdidi mara nyingi hutofautisha kati ya maneno yasiyohusiana. Kama ilivyo kwa Kiitaliano, Kinorwe hutumia fupi kabla ya konsonanti mbili zilizoongozana na irabu ndefu kabla ya konsonanti moja. Kuna tofauti kati ya irabu fupi na ndefu:
- måte [ˈmôːtə] / måtte [ˈmɔ̂tːə] – 'mbinu' / 'lazima'
- lete [ˈlêːtə] / lette [ˈlɛ̂tːə] – 'kutafuta' / 'kuondoka'
- sine [ˈsîːnə] / sinne [ˈsɪ̂nːə] – 'yao' / 'hasira'
Kirusi
haririKwa Kirusi, urefu wa konsonanti unaonyeshwa kwa herufi mbili, kama ilivyo kwa ванна [ˈvannə] 'bafu'). Hii inaweza kutokea katika hali kadhaa.
Kihispania
haririKuna konsonanti za tashdidi katika Kihispania cha Karibea kutokana na unyambulishaji wa /l/ na /ɾ/ katika konsonanti ya silabi kwa konsonanti zifuatazo. [10] Mifano ya Kihispania cha Kuba:
/l/ au /r/ + /f/ | → | [ff] | a[ff]iler, hue[ff]ano | (Sp. alfiler, huérfano ) |
/l/ au /r/ + /h/ | → | [ɦh] | ana[ɦh]ésico, vi[ɦh]en | (Sp. analgésico, virgen) |
/l/ au /r/ + /b/ | → | [bb] | si[bb]a, cu[bb]a | (Sp. silba au sirva, curva) |
/l/ au /r/ + /d/ | → | [DD] | ce[dd]a, acue[dd]o | (Sp. celda au cerda, acuerdo) |
/l/ au /r/ + /g/ | → | [gg] | pu[gg]a, la[gg]a | (Sp. pulga au purga, larga) |
/l/ au /r/ + /m/ | → | [mm] | ca[mm]a, a[mm]a | (Sp. calma, alma au arma) |
/l/ au /r/ + /n/ | → | [nn] | pie[nn]a, ba[nn]eario | (Sp. pierna, balneario) |
/l/ au /r/ + /l/ | → | [ll] | bu[ll]a, cha[ll]a | (Sp. burla, charla) |
Kiganda
haririKiganda si cha kawaida kwa kuwa tashdidi inaweza kutokea sehemu ya neno-awalii, pamoja na neno-kati. Kwa mfano, /kːapa/ kkapa 'paka', /ɟːaɟːa/ jjajja 'babu' na /ɲːabo/ nnyabo 'bibiye' zote huanza na konsonanti yenye tashdidi.
Kuna konsonanti tatu ambazo haziwezi kuwa na tashdidi: /j/, /w/ na /l/. Wakati wowote kanuni za kimofolojia zinapohitaji kuzipa tashdidi konsonanti hizi, /j/ na /w/ zinaainishwa na /ɡ/, na /l/ hadi /d/. Kwa mfano:
- -ye /je/ 'army' (root) > ggye /ɟːe/ 'an army' (noun)
- -yinja /jiːɲɟa/ 'stone' (root) > jjinja /ɟːiːɲɟa/ 'a stone' (noun); jj is usually spelt ggy
- -wanga /waːŋɡa/ 'nation' (root) > ggwanga /ɡːwaːŋɡa/ 'a nation' (noun)
- -lagala /laɡala/ 'medicine' (root) > ddagala /dːaɡala/ 'medicine' (noun)
Kijapani
haririKatika Kijapani, urefu wa konsonanti ni bainifu (kama vile urefu wa irabu). Tashdidi katika mfumo wa maandshi silabario huwakilishwa na sokuon, tsu ndogo : [11]っ kwa hiragana kwa maneno asilia naッ kwa katakana kwa maneno ya kigeni. Kwa mfano,来た (きた, kita) maana yake 'alikuja; alifika', huku 切った (きった , kitta ) maana yake ni 'kata;'. Pamoja na utitiri wa gairaigo ('maneno ya kigeni') katika Kijapani cha Kisasa, konsonanti zinazotamkwa zimeweza kupata tashdidi pia: [12]バグ ( bagu) inamaanisha '(kompyuta) mdudu', na バッグ ( baggu) maana yake ni 'mfuko'. Tofauti kati ya tashdidi usio na sauti na wenye sauti inaonekana katika jozi za maneno kama vileキット ( kitto, ikimaanisha 'seti') na キッド ( kiddo, ikimaanisha 'mtoto'). Pia, katika mazungumzo ya Kijapani cha Kisasa, tashdidi inaweza kutumika kwa baadhi ya vivumishi na vielezi ili kuongeza msisitizo: すごい ( sugoi, 'staajabu') inatofautiana na すっごい ( suggoi, 'staajabu sana ') ;思い切り (おもいきり, omoikiri, 'kwa nguvu zote') inatofautiana na 思いっ切り (おもいっきり, omoikkiri, ' kweli kwa nguvu zote').
Kituruki
haririKatika Kituruki tashdidi inaonyeshwa kwa herufi mbili zinazofanana kama katika lugha nyingi.
- anne [annɛ]
- hürriyet [çyɹ̝ːije̝t]
Tashnida pia hutokea wakati kiambishi kinachoanza na konsonanti kinapokuja baada ya neno linaloishia na konsonanti sawa.
- el [el] ('mkono') + -ler [læɾ̥] (inaashiria wingi) = eller [eˈlːæɾ̥] ('mikono'). (linganisha na eler, 'anatengua')
- at [at] ('kurusha') + -tık [tɯk] ("inaashiria wakati uliopita, nafsi ya kwanza wingi) = attık [aˈtːɯk] ('tulirusha'). (linganisha na atık, 'waste')
Lugha za Kidravidi
haririKimalayalam
haririKatika Kimalayalam, ujumuishaji una hali ya kifonolojia [13] inayoitwa sandhi na tashdidi hutokea katika mipaka ya maneno. Sandhi ya tashdidi inaitwa dvitva sandhi au 'sandhi maradufu'.
Mfano:
- മേശ + പെട്ടി (mēśa + peṭṭi) – മേശപ്പെട്ടി (mēśappeṭṭi)
Tashdidi pia hutokea katika mofimu moja kama കള്ളം (kaḷḷaṁ) ambayo ina maana tofauti na കളം (kaḷaṁ).
Uandishi
haririKatika lugha iliyoandikwa, urefu wa konsonanti mara nyingi huonyeshwa kwa kuandika konsonanti mara mbili (ss, kk, pp, na kadhalika), lakini pia unaweza kuonyeshwa kwa ishara maalum, kama vile shadda katika Kiarabu, dagesh katika Kiebrania cha Kale, au sokuon katika Kijapani .
Katika Alfabeti ya Kifonetiki ya Kimataifa, konsonanti ndefu kwa kawaida huandikwa kwa kutumia koloni ya pembe tatu ː, mfano penne [penːe] ('manyoya', 'kalamu', pia aina ya tambi), ingawa herufi zilizoongezwa maradufu pia hutumika (hasa kwa maumbo ya msingi ya fonimu, au katika lugha zenye toni ili kuwezesha uwekaji alama za herufi).
Marejeo
hariri- ↑ Mitterer, Holger (2018-04-27). "The singleton-geminate distinction can be rate dependent: Evidence from Maltese". Laboratory Phonology (kwa Kiingereza). 9 (1). Association for Laboratory Phonology: 6. doi:10.5334/labphon.66.
- ↑ 2.0 2.1 William Ham, Phonetic and Phonological Aspects of Geminate Timing, p. 1–18
- ↑ 3.0 3.1 Blust, Robert. (2013). The Austronesian Languages (Rev. ed.). Australian National University.
- ↑ Yupho, Nawanit (6 Februari 1989). "Consonant Clusters and Stress Rules in Pattani Malay". Mon-Khmer Studies: 129–133 – kutoka SEAlang.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Nawawi, Nazarina (14 Januari 2013). "Kajian Dialek Trengganu". slideshare (kwa Kimalei). Iliwekwa mnamo 7 Juni 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Jackson, Geoff and Jenny (1999). An introduction to Tuvaluan. Suva: Oceania Printers.
- ↑ Ben Hedia S (2019). Gemination and degemination in English affixation: Investigating the interplay between morphology, phonology and phonetics (pdf). Berlin: Language Science Press. doi:10.5281/zenodo.3232849. ISBN 978-3-96110-188-7.
- ↑ "Raddoppiamenti di vocali e di consonanti". Dizionario italiano d'ortografia e pronunzia (DOP). RAI. 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 30, 2018. Iliwekwa mnamo Novemba 11, 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Khatiwada, Rajesh (Desemba 2009). "Nepali". Journal of the International Phonetic Association (kwa Kiingereza). 39 (3): 373–380. doi:10.1017/S0025100309990181. ISSN 0025-1003.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Arias, Álvaro (2019). "Fonética y fonología de las consonantes geminadas en el español de Cuba". Moenia. 25, 465-497
- ↑ Asano, Yoshiteru (1994). "Mora-Based Temporal Adjustments in Japanese" (en). Colorado Research in Linguistics (kwa Kiingereza). 13. University of Colorado Boulder. p2 line 29. doi:10.25810/2ddh-9161.
- ↑ Kawahara, Shigeto (2006), "A Faithfulness ranking projected from a perceptibility scale: The case of [+ Voice] in Japanese" (PDF), Language, juz. 82, na. 3, Linguistic Society of America, ku. 536–574, doi:10.1353/lan.2006.0146, p. 538
- ↑ Inkelas, Sharon (2014). The Interplay of Morphology and Phonology. Oxford Surveys in Syntax & Morphology. Oxford University Press. uk. 10. ISBN 9780199280476.