Utendaji (serikali)

(Elekezwa kutoka Tawi la utendaji)

Tawi la Utendaji, pia mkono wa utendaji, ni tawi la serikali ambalo hutendesha mamlaka ya serikali. Katika mifumo ya kisiasa iliyotengenezwa kutumia kanuni za utengano wa nguvu, mamlaka yamegawiwa kati ya matawi ya utendaji, bunge na mahakama, ili kuzuia kukolea kwa nguvu kati ya kikundi kidogo cha watu. Katika mfumo huo, kazi ya utendaji ni kutekeleza sheria kama iliyoandikwa na bunge na kuelezewa na mahakama[1][2]. Tawi la utendaji linaweza kutoa amri za utendaji, kifalme au rais ambazo ni aina ya sheria. Serikali na taasisi zake kama vile, Mashirika ya umma, tume, kamati, halmashauri au bodi (ambazo huwa sehemu ya utendaji), zinaweza kuandika kanuni ambazo pia ni aina ya sheria.

Mkono wa utendaji huwa na viongozi wafuatao:

Marejeo

hariri
  1. History.com staff, "THREE BRANCHES OF GOVERNMENT", History.com, ilipatikana mnamo 27-03-2018
  2. "THE STRUCTURE OF GOVERNMENT IN THE CONSTITUTION OF KENYA 2010", Chuo Kikuu Cha Nairobi, ilipatikana mnamo 27-03-2018