Teresa wa Yesu Jornet

(Elekezwa kutoka Teresa Jornet Ibars)

Teresa wa Yesu Jornet (jina la kuzaliwa: Teresa Jornet Ibars; Aitona, Lerida, 9 Januari 1843 - Liria, Valencia, 26 Agosti 1897) alikuwa bikira wa Kanisa Katoliki nchini Hispania ambaye alianzisha shirika lake lijulikanalo kama Dada Wadogo wa Wazee Waliotelekezwa kwa ajili ya kuhudumia watu wa namna hiyo [1].

Sanamu yake huko Valencia.

Ibars alikuwa mpwa wa Francisco Palau na rafiki wa karibu wa Saturnino López Novoa. Alijitolea sana kuhudumia wazee na wagonjwa, kazi iliyojulikana na kuthaminiwa, huku shirika lake likieneza huduma zake Hispania na hatimaye nje ya nchi.

Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 27 Aprili 1958 katika Basilika la Mtakatifu Petro, halafu Papa Paulo VI akamtangaza mtakatifu tarehe 27 Januari 1974[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91058
  2. "Saint Teresa of Jesus Jornet Ibars - Newman Connection - Effingham, IL". www.newmanconnection.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-01. Iliwekwa mnamo 2020-07-24.
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.