Teresa wa Yesu Jornet
Teresa wa Yesu Jornet (jina la kuzaliwa: Teresa Jornet Ibars; Aitona, Lerida, 9 Januari 1843 - Liria, Valencia, 26 Agosti 1897) alikuwa bikira wa Kanisa Katoliki nchini Hispania ambaye alianzisha shirika lake lijulikanalo kama Dada Wadogo wa Wazee Waliotelekezwa kwa ajili ya kuhudumia watu wa namna hiyo [1].
Ibars alikuwa mpwa wa Francisco Palau na rafiki wa karibu wa Saturnino López Novoa. Alijitolea sana kuhudumia wazee na wagonjwa, kazi iliyojulikana na kuthaminiwa, huku shirika lake likieneza huduma zake Hispania na hatimaye nje ya nchi.
Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 27 Aprili 1958 katika Basilika la Mtakatifu Petro, halafu Papa Paulo VI akamtangaza mtakatifu tarehe 27 Januari 1974[2].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/91058
- ↑ "Saint Teresa of Jesus Jornet Ibars - Newman Connection - Effingham, IL". www.newmanconnection.com. Iliwekwa mnamo 2020-07-24.
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Hermanitas de los ancianos desamparados Tovuti rasmi ya shirika lake
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |