Theodora Guerin (Étables-sur-Mer, Ufaransa, 2 Oktoba 1798 - Saint Mary-of-the-Woods, Indiana, Marekani, 14 Mei 1856) alikuwa sista wa Ufaransa ambaye alitumwa na wenzake watano kuanzisha jumuia ya shirika lao huko Marekani[1][2] aliposhughulikia kwa huruma hasa malezi ya wasichana akitegemea daima Maongozi ya Mungu [3][4].

Baadaye tawi hilo lilitengwa na shirika mama, hivyo Theodora akahesabiwa kama mwanzilishi[5][6].

Alitangazwa rasmi mwenyeheri na Papa Yohane Paulo II tarehe 25 Oktoba 1998, halafu mtakatifu na Papa Benedikto XVI 15 Oktoba 2006.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyofariki dunia[7].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.