Thori
Thori (thorium) ni elementi ya kimetali yenye alama Th na namba atomia 90.
Thori (Thorium) | |
---|---|
Kipande kidogo cha bati cha Thori, iliyofungwa katika gesi ya Arigoni (inayozuia kuoksidika)
| |
Jina la Elementi | Thori (Thorium) |
Alama | Th |
Namba atomia | 90 |
Mfululizo safu | Aktinidi |
Uzani atomia | 232.0377 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 18, 10, 2 |
Densiti | 10 g/cm³ (kadirio) |
Ugumu (Mohs) | 3.0 |
Kiwango cha kuyeyuka | °K 2023 |
Kiwango cha kuchemka | °K 5061 |
Asilimia za ganda la dunia | ppm 11 |
Hali maada | mango |
Mengineyo | nururifu |
Thori safi ni metali laini yenye rangi ya kifedha-kijivu; baada ya kukaa hewani inaelekea polepole kuwa nyeusinyeusi.
Iligunduliwa Norwei na kupewa jina lake Uswidi mwaka 1829. Jina la Thori limechukuliwa kutoka mungu wa ngurumu wa Skandivia ya Kale.
Thori ni elementi yenye unururifu dhaifu. Isotopi yake ya 232Th ina nusumaisha ya miaka bilioni 14.05 inayozidi hata umri wa Dunia. Wanajiolojia hukadiria kuwa mbunguo nyuklia wa Thori unachangia sana katika joto lililopo ndani ya Dunia[1].
Inapatikana kiasili katika madini, hasa Uhindi, Marekani na Australia. Akiba zake ni kubwa kushinda urani, kwa hiyo kuna majadiliano kama itafaa kutumiwa kwa tanuri nyuklia baada ya kumaliza akiba za urani[2]. Lakini kuna pia wasiwasi kwa sababu inaonekana si thabiti kama urani katika mchakato wa mwatuko nyuklia, hivyo kuna hofu ya ajali pamoja na hatari ya matumizi ya thori kutoka tanuri kwa ajili ya silaha za nyuklia[3].
Marejeo
hariri- ↑ Gando, A.; Gando, Y.; Ichimura, K.; et al. (2011). "Partial radiogenic heat model for Earth revealed by geoneutrino measurements" (PDF). Nature Geoscience. 4 (9): 647–651. Bibcode:2011NatGe...4..647K. doi:10.1038/ngeo1205.
- ↑ Thorium, tovuti ya World Nuclear Association (shirika la tasnia ya kinyuklia), iliangaliwa Machi 2020
- ↑ Stephen F. Ashley, Geoffrey T. Parks, William J. Nuttall, Colin Boxall, Robin W. Grimes: Thorium fuel has risks. In: Nature. Band 492, Nr. 7427, 6. Dezember 2012, S. 31–33, doi:10.1038/492031a
Tovuti za Nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Thori kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |