Ubuntu
Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Falsafa hiyo inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kuliko ubinafsi.
Neno Ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na Kixhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwa Kiswahili "Utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana hiyohiyo.
Falsafa ya Ubuntu imetokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi ya jamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi.
Msingi wa falsafa hiyo ni kamba, "mtu si mtu bila watu" (kwa Kizulu, "Umuntu ngumuntu ngabantu"; kwa Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu". Baadhi ya watu wanaiona falsafa ya Ubuntu kuwa na maana nzito ya kiroho na ya kidini kwa kuwa imejengwa juu ya upendo kwa watu wengine na hata kwa mazingira.
Viungo vya Nje
hariri- ubuntu: Falsafa ya Kiafrika
- Ubuntu na Sheria Afrika Kusini
- Bill Clinton Akisisitiza Kuhusu Ubuntu
- video Archived 24 Januari 2021 at the Wayback Machine.
- Makala Kuhusu Ubuntu na Dini
- Tafsiri ya Ubuntu Toka Kwa Askofu Desmond Tutu Archived 6 Aprili 2017 at the Wayback Machine.
- Video: Mandela Akitafsiri Ubuntu Archived 8 Novemba 2006 at the Wayback Machine.
- Video ya Mandela Akizungumzia Ubuntu Archived 28 Novemba 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ubuntu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |