Ummy Ally Mwalimu
Ummy Ally Mwalimu (alizaliwa 5 Septemba 1973) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama tawala cha kisiasa [1].
Mheshimiwa Ummy Mwalimu Mb | |
Waziri Wizara ya Nchi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
| |
Aliingia ofisini 12 Desemba 2015 | |
Rais | John Magufuli |
---|---|
Naibu Waziri wa Mazingira
| |
Muda wa Utawala 30 Januari 2014 – 5 Novemba 2015 | |
mtangulizi | Charles Kitwanga |
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Jinsia, Wazee na Watoto
| |
Muda wa Utawala 28 Novemba 2010 – 20 Januari 2014 | |
aliyemfuata | Pindi Chana |
Aliingia ofisini Novemba 2010 | |
Constituency | Hana jimbo (Mbunge wa viti maalumu) |
tarehe ya kuzaliwa | 5 Septemba 1973 |
utaifa | Tanzanian |
chama | CCM |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (LL.B) University of Pretoria (LL.M) |
Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2015. Akarudishwa tena bungeni[2]
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia tiketi ya CCM Viti Maalum vya Wanawake 2015.
Mwaka 2017 aliteuliwa kuwa waziri katika Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Archived 30 Juni 2020 at the Wayback Machine.[3] Mwaka 2021 aliteuliwa na raisi wa sita wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan kuwa waziri katika wizara ya Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Elimu na kazi
Ummy Mwalimu[4] alihitimu elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Archived 10 Desemba 2021 at the Wayback Machine. mwaka 1998.
Alitunukiwa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998. Mwaka 2001 alitunukiwa shahada ya uzamili ya sheria katika chuo kikuu cha Pretoria. Ummy Mwalimu amefanya kazi sehemu mbalimbali serikalini na katika mashirika yanayojihusisha na tafiti kuhusu sheria, uongozi unaozingatia Sheria na Utawala Bora.
Uzoefu katika siasa
Ummy Mwalimu ameshika nafasi mbalimbali katika ulingo wa siasa. Mwaka 2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na mwaka 2014-2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Mwaka 2015 alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Sheria na Katiba, mwaka 2014/5 alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mazingira na mwaka 2010-2014 alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.[4]
Pia Ummy Mwalimu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili (2010 hadi 2015 na mwaka 2015 hadi 2020) kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Viti Maalum kwa Wanawake.
Mwaka 2007-2015 Ummy alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga na mwaka 2008 hadi 2015 alikuwa mjumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) Tanga.[4] Mwalimu ameshika nafasi nyingi za uongozi katika chama na serikali.
Mapambano dhidi ya Korona
Ummy Mwalimu amepata umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu maarufu unaotokana na virusi vya Corona, kwa jina la kitaalamu COVID 19 ambao uliingia nchini Tanzania tarehe 15 Machi 2020 [5][6]. Ummy amechukua tahadhari wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgonjwa huyo ili kuzuia taharuki na hofu kwa wananchi. Ummy amezingatia weledi na kanuni za kukabiliana na majanga, jambo ambalo limewawezesha Watanzania kuendelea kufanya kazi bila hofu. Hivi karibuni Mwalimu alisema kuwa ugonjwa wa korona umepungua na kuwataka Watanzania kuendelea na shughuli zao huku wakichukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo [7].
Marejeo
- ↑ Chama Cha Mapinduzi (CCM)
- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017]
- ↑ About The Ministry Archived 6 Juni 2017 at the Wayback Machine., tovuti ya wizara, iliangaliwa Juni 2017
- ↑ 4.0 4.1 4.2 "Parliament of Tanzania". www.parliament.go.tz. Iliwekwa mnamo 2020-06-30.
- ↑ [1]
- ↑ "VIDEO: Tanzania confirms first Coronavirus case in Arusha". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-06-30.
- ↑ [2]
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |