Vladimir Lenin

Vladimir Ilyich Lenin (Влади́мир Ильи́ч Ле́нин) alikuwa na jina la kiraia Vladimir Ilyich Ulyanov (Влади́мир Ильи́ч Улья́нов) (*10 Aprili (22 Aprili ya kalenda ya Gregori) 1870 - + 21 Januari 1924) alikuwa mwanasiasa nchini Urusi na kiongozi wa chama cha Bolsheviki akaendesha awamu la kikomunisti la Mapinduzi ya Urusi ya 1917 akaanzisha Umoja wa Kisovyeti. Mafundisho yake yalikuwa msingi wa itikadi ya Ulenin.

Lenin akihotubia wananchi
Kaburi la Lenin mbele ya ukuta wa Kremlini mjini Moskva

Lenin alizaliwa katika familia tajiri katika mji wa Simbirsk, (sasa unaitwa Ulyanovsk), Lenin alianza kupendelea mapinduzi baada ya kaka yake kuuliwa mwaka wa 1887. Alipofukuzwa kutoka Chuo Kikuu cha Kazan kwa maandamano ya kuipinga serikali ya Tsar, alijishughulisha kupata shahada ya sheria katika miaka iliyoufuata.

Alianza kutumia jina la "Lenin" kama jina la siri alipojiunga na upinzani dhidi ya serikali ya kifalme ya Kirusi. Hakuna uhakika kama alilitumia kama kumbukumbu kwa mlezi wake alipokuwa mtoto au kutokana na mto Lena katika jimbo la Siberia alipohamishwa ufungoni 1897 baada ya kushiriki katika upinzani dhidi ya serikali.

Lenin aliaga dunia mjini Nizhny Novgorod (Gorki karibu na Moskva) tar. 21 Januari 1924. Maiti yake ilihifadhiwa kwa madawa na kuonyeshwa katika kaburi kubwa kwenye uwanja nyekundu mjini Moskva. Kiongozi aliyemfuata alikuwa Josef Stalin.

Crystal personal.svg Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vladimir Lenin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.