Masafa ya mawimbi

(Elekezwa kutoka Urefu wa wimbi)

Masafa ya mawimbi (pia urefu wa wimbi[1], mara chache lukoka[2]; kwa Kiingereza wavelength) ni namna ya kupima na kutaja ukubwa wa wimbi.

Picha inaonyesha mawimbi kwenye bahari; alama ya λ inaonyesha umbali kati ya vilele viwili au masafa ya mawimbi. Herufi ya Kigiriki λ Lambda ni alama ya urefu wa wimbi.
Lukoka au urefu wa wimbi hupimwa kati ya sehemu zinazolingana ya mawimbi mawili.

Ni umbali kati ya sehemu za kulingana za mawimbi mawili ambayo yanafuatana, kwa mfano kati ya kilele na kilele au mabonde yao.

Mawimbi yapo kila sehemu ya mazingira asilia, kwa mfano:

Masafa ya mawimbi hutofautiana sana. Mawimbi marefu yanayoweza kutambuliwa na milango ya fahamu ya binadamu ni sauti ya besi yenye masafa ya mita 21. Sikio letu linatambua mawimbi yenye masafa kati ya milimita 17 hadi mita 21.

Mawimbi sumakuumeme yana upeo mkubwa.

Masafa ya mawimbi na marudio

hariri

Masafa ya mawimbi huwa na uhusiano wa kinyume na marudio ya wimbi. Kama marudio ya wimbi ni ya juu, masafa yake yatakuwa madogo. Vilevile kinyume, kama wimbi lina masafa makubwa, marudio yake ni madogo.

Marejeo

hariri
  1. Kamusi ya TUKI
  2. Lukoka ni pendekezo la KAST, 1995 lisilotumika sana

Tovuti za Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: