Uwanja wa michezo wa Mbombela
Uwanja wa michezo wa Mbombela ni uwanja wa michezo wa shirikisho la mpira wa miguu na umoja wa michezo ya raga(rugby) unaopatikana Mbombela, hapo zamani palifahamika kama Nelspruit katika jimbo la Mpumalanga, Afrika Kusini. Ulijengwa kwa ajili ya kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2010. Ni moja wapo ya viwanja 10 vilivyotumika kwa michezo ya soka na moja kati ya viwanja 5 vipya vilivyo jengwa kwa ajili ya kombe la dunia la mwaka 2010. Ni uwanja wa nyumbani kwa klabu ya Pumas na unauwezo wa kubeba washabiki 40,929 na wote wakiketi kwenye viti.[1]
Unapatikana kilomita sita(6) magharibi mwa jimbo la Mpumalanga na ndio uwanja mkubwa kuliko vyote katika hilo jimbo. Kiasi cha R1,050-milioni kilitumika kujenga uwanja huu na uwanja ulikuwa tayari kabla ya Juni 2010 na fedha zote zilitolewa na serikali kuu kupitia mapato ya ushuru na hapakuwa na kiasi chochote cha fedha kilichohitajika kutoka halmashauri ya jiji.
Matokeo ya MashindanoEdit
Kombe la Dunia la FIFA 2010Edit
Tarehe | Muda (UTC+2) | Timu # 1 | Matokeo | Timu # 2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|---|
16 Juni 2010 | 13:30 | [[Image:|22x20px|border|Bendera ya Honduras]] Honduras | 0–1 | Chile | Kundi H | 32,664 |
20 Juni 2010 | 16:00 | Italia | 1–1 | New Zealand | Kundi F | 38,229 |
23 Juni 2010 | 20:30 | Australia | 2–1 | Serbia | Kundi D | 37,836 |
25 Juni 2010 | 16:00 | North Korea | 0–3 | Ivory Coast | Kundi G | 34,763 |
Kombe la mataifa Afrika 2013Edit
Tarehe | Muda (UTC+2) | Timu # 1 | Matokeo | Timu # 2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|---|
21 Januari 2013 | 17:00 | Zambia | 1–1 | Ethiopia | Kundi C | 15,500 |
21 Januari 2013 | 20:00 | Nigeria | 1–1 | Burkina Faso | Kundi C | 13,500 |
25 Januari 2013 | 17:00 | Zambia | 1–1 | Nigeria | Kundi C | 25,000 |
25 Januari 2013 | 20:00 | Burkina Faso | 4–0 | Ethiopia | Kundi C | 35,000 |
29 Januari 2013 | 19:00 | Zambia | 0–0 | Burkina Faso | Kundi C | 8,000 |
30 Januari 2013 | 18:30 | Togo | 1–1 | Tunisia | Kundi D | 7,500 |
3 Februari 2013 | 18:30 | Burkina Faso | 1–0 (Muda wa ziada) | Togo | Robo fainali | 27,000 |
6 Februari 2013 | 18:30 | Burkina Faso | 1–1 (Muda wa ziada) (3–2 pen.) | Ghana | Nusu fainali | 30,000 |
Mechi ya ufunguziEdit
Mnamo tarehe 16 Mei 2010, uwanja ulizinduliwa rasmi kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Afrika Kusini na timu ya taifa ya Thailand. Afrika Kusini walishinda 4–0, wakiongoza 3–0 katika kipindi cha kwanza.
MarejeoEdit
- ↑ Mbombela Stadium: the stadiums for the 2010 FIFA World Cup South Africa. FIFA.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-08-26. Iliwekwa mnamo 2021-06-09.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Mbombela kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |