Honduras ni nchi ya Amerika ya Kati. Imepakana na Guatemala, El Salvador na Nikaragua. Upande wa kusini ina pwani fupi ya Pasifiki na upande wa kaskazini pwani ndefu ya Bahari ya Karibi.

República de Honduras
Jamhuri ya Honduras
Bendera ya Honduras Nembo ya Honduras
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Libre, Soberana e Independiente
Wimbo wa taifa: „Tu bandera es un lampo de cielo“
(wewe bendera u nuru ya angani)
Lokeshen ya Honduras
Mji mkuu Tegucigalpa
14°6′ N 87°13′ W
Mji mkubwa nchini Tegucigalpa
Lugha rasmi Kihispania
Serikali Jamhuri, demokrasia
Xiomara Castro
Uhuru
Imetangazwa
imetambuliwa

15 Septemba 1821
1823
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
112,412 km² (ya 101)
(kidogo sana)
Idadi ya watu
 - 2018 kadirio
 - 2022 sensa
 - Msongamano wa watu
 
9,587,522 (ya 95)
9,540,539
84.72/km² (ya 128)
Fedha Lempira (HNL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-6)
(UTC)
Intaneti TLD .hn
Kodi ya simu +504

-


Jiografia

hariri
 
Ramani ya Honduras

Honduras ni nchi ya milima mingi inayopanda hadi kimo cha Cerro Las Minas chenye mita 2849 juu ya UB.

Mito mingi ya Honduras huelekea Atlantiki. Río Patuca na Río Ulúa ndiyo mito mirefu ya nchi.

Ziwa kubwa ni Lago de Yojoa lenye eneo la km² 285: ni muhimu kwa ajili ya maji ya miji.

Hali ya hewa ni ya kitropiki lakini joto linapoa milimani.

Mji mkuu na mji mkubwa wenye wakazi milioni 1.09 ni [Tegucigalpa]].

Miji mingine mikubwa kiasi ni San Pedro Sula (wakazi 491,000) katika kaskazini-magharibi, halafu miji ya bandari ya La Ceiba (wakazi 111,000) na Puerto Cortés (wakazi 36,000).

Historia

hariri

Honduras ilikuwa sehemu ya maeneo ya Wamaya. Lakini miji yao ilikwaisha tayari kabla ya kufika kwa Wahispania. Kristoforo Kolombo alifika mwaka 1502 karibu na Trujillo katika kaskazini na kuita nchi "Honduras" (kwa Kihispania "vilindi") kwa sababu ya maji marefu mwambaoni.

Miaka 1524 na 1525 Wahispania walianza kuvamia nchi wakaunda mji wa Comayagua mwaka 1540. Mji mkuu wa leo ulianzishwa mwaka 1579 kama kituo cha kuchimba madini kama dhahabu na fedha.

Mwaka 1821 Honduras ilijiunga na ghasia ya maeneo mengine ya Amerika ya Kati dhidi ya utawala wa Hispania. Mwanzoni nchi hizo ndogo zilijiunga na Meksiko lakini baada ya miaka miwili zilianzisha "Shirikisho la Amerika ya Kati" lililokwisha mwaka 1839.

Tangu mwaka ule Honduras imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.

Wakazi

hariri
 
Kanisa Kuu la Tegucigalpa lilijengwa wakati wa utawala wa Wahispania.

Idadi ya wakazi ni zaidi ya milioni 8.

Wakazi walio wengi kabisa (90%) ni machotara hasa wenye asili ya mchanganyiko wa Waindio na Wazungu. Hao ndio asilimia 90 ya wakazi wote. Katika misitu ya milimani kuna bado vikundi vya wenyeji asilia (Wahindi wekundu, 7%). Wengine ni wa asili ya Afrika (2%) au ya Ulaya (1%) wasiochanganyika sana na wengine. Kwenye pwani ya kaskazini kuna makazi ya Wagarifuna ambao wana utamaduni wa mchanganyiko wa Wahindi wekundu na Waafrika.

Upande wa lugha, Kihispania ndiyo lugha rasmi, lakini lugha za wakazi asili zinatambulika pia kisheria.

Upande wa dini, karibu wote ni wafuasi wa Yesu katika Kanisa Katoliki (walau 46-47%), lakini pia katika madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Honduras kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.