Vinsenti Pallotti

mitalia Mroma Mkatoliki na mtume

Vinsenti Pallotti (Roma, Italia, 21 Aprili 1795 – Roma, 22 Januari 1850) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanzilishi wa Shirika la Utume Katoliki.

Picha ya Mt. Vinsenti Pallotti.

Kwa maandishi yake na kwa miundo ya namna hiyo aliyoianzisha alichochea wito wa Wakristo wote wa kulifanyia Kanisa kazi kwa bidii.

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 22 Januari 1950, halafu mtakatifu na Papa Yohane XXIII tarehe 20 Januari 1963.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Januari[1].

Tanbihi hariri

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.