Vita ya Krim (1853-1856; kwa Kiing. Crimean War) ilikuwa vita iliyopigwa kati ya Urusi upande mmoja na Ufaransa, Uingereza, Ufalme wa Sardinia na Milki ya Osmani upande mwingine. Mapigano mengi yalitokea kwenye rasi ya Krim katika Bahari Nyeusi, lakini mengine yalitokea pia magharibi mwa Uturuki na karibu na Bahari ya Baltiki.

Mashambulio ya kikosi cha farasi cha Kiingereza wakati wa Vita ya Krim.

Vita ya kisasa ya kwanza

hariri
 
Bahari Nyeusi na milki zilizoizunguka kabla ya vita ya Krim; Krim ni rasi kaskazini mwa bahari.

Wakati mwingine vita hiyo imeitwa "vita ya kisasa" ya kwanza, kwa sababu ya matumizi ya silaha, pamoja na mikakati, ambayo hayakuwa kawaida hadi sasa na ikaendelea kuathiri vita zilizofuata.[1] Ilikuwa pia vita vya kwanza iliyoripotiwa moja kwa moja kwa njia ya telegrafu na kuchapishwa kwenye magazeti ya Ulaya. Habari hizo zilionyesha mara ya kwanza mateso ya wajeruhiwa na vifo vyao kutokana na maandalizi mabaya ya uongozi wa kijeshi na kusababisha mbinu mpya za tiba ya kijeshi. [2] Matumizi ya telegrafu yaliwawezesha viongozi wa kijeshi kupeana habari haraka na kuwasiliana na serikali zao. Silaha mpya zilitumiwa mara ya kwanza vitani kama vile mabomu ya kutega baharini, manowari za ubao zilizofunikwa kwa mabamba ya chuma na kuendeshwa kwa injini za mvuke; bunduki za askari zilizotengenezwa kiwandani na risasi mpya zilizoruhusu kipiga haraka zaidi na kulenga kwa umbali mkubwa. Uharibifu mkubwa uliosababishwa na silaha mpya ulilazimisha mikakati mipya ya kijeshi, kama vile matumizi ya handaki badala ya mapigano ya wazi. Matumizi ya reli yaliwapa Waingereza na Wafaransa faida kubwa, na ukosefu wake upande wa Urusi uliongeza matatizo yao.

Baada ya vita hiyo ilieleweka kwamba uchumi wa taifa na tekinolojia vinaweza kuwa na umuhimu mkubwa kuliko idadi ya askari.

Mandharinyuma

hariri

Nguvu ya Milki ya Osmani ilikuwa ikipungua katika karne ya 19. Sultani alipaswa kukubali uhuru wa Ugiriki na Serbia; Misri iliwahi kutangaza uhuru wake chini ya Muhamad Ali Pasha hadi kuvamia Uturuki mnamo 1833. Nchi za Ulaya zilingilia kati na kuokoa Waosmani. Wakati huohuo, nguvu ya Urusi ilikuwa ikiongezeka na katika mfululizo wa vita kadhaa Urusi ilitwaa milima ya Kaukazi, ufuko wa kaskazini ya Bahari Nyeusi na maeneo kadhaa ya Balkani yaliyowahi kutawaliwa na Waosmani. Uingereza ilihofia kuenea kwa Urusi hadi Bahari ya Mediteranea hivyo ikaona afadhali kusimama upande wa Waosmani.

Ugomvi ulioleta vita ya krimea ulianza kutokana na mashindano kati ya Urusi na Ufaransa kuhusu kipaumbele kama mlinzi wa maslahi ya Wakristo katika Yerusalemu ya Kiosmani na hasa kuhusu Kanisa la Kuzaliwa kwa Kristo mjini Bethlehemu ambako kila upande ulidai nafasi ya kwanza. [3]

Sultani wa Waosmani alitishiwa kutambua mara Urusi, mara Ufaransa kama "mlinzi wa Wakristo" katika nchi takatifu. Tsar (mfalme) Aleksander wa Urusi alikasirika akatuma jeshi lake kwenda majimbo mawili ya Kiosmani huko Romania ya leo; Wafaransa na Waingereza walituma manowari kwenye Bahari ya Aegaean karibu na Dardaneli kama onyo.

Nchi jirani Austria na Prussia ziliamua kutoshiriki katika vita.

Mwendo wa vita

hariri
 
Bahari Nyeusi wakati wa mashambulio ya Uingereza na Ufaransa kwenye Rasi ya Krim (zambarau: Milki ya Osmani (Empire Ottoman); kijani: Urusi (Empire Russe); kahawia: Austria (Empire Autrichien); mshale mwekundu: mashambulio ya jeshi la Uingereza na Ufaransa

Serikali ya sultani ilitaka Warusi waondoke tena katika majimbo ya Balkani lakini Warusi walikataa. Hivyo, baada ya kushauriana na Uingereza na Ufaransa, Milki ya Osmani ilitangaza vita dhidi ya Urusi.

 
Mapigano katika Anatolia ya Mashariki kati ya Waosmani na Warusi mnamo 1853-1855

Kwenye mapigano ya kwanza Warusi walishindwa lakini manowari zao zilifaulu kwenye Novemba 1853 kuzamisha jeshi la majini la Waosmani kwenye Bahari Nyeusi. Uingereza na Ufaransa zilituma manowari zao kupitia mlango wa Bosporus hadi Bahari Nyeusi. Baada ya majadiliano kati ya mabalozi hayakufikia popote, nchi hizo mbili zilitangaza vita dhidi ya Urusi kwenye Machi 1854.

Mapigano yalianza sasa katika maeneo mbalimbali ya mipaka ya Urusi, pamoja na Bahari Baltiki, Rasi ya Balkani, Anatolia ya Mashariki na kwenye Rasi ya Kamchatka. Lakini kitovu cha vita kilikuwa mashambulio dhidi ya bandari ya Sevastopol kwenye Rasi ya Krim.

Mapigano yaliendelea kwa muda mrefu; Waingereza na Wafaransa pamoja na vikosi vya Waosmani na Waitalia walishambulia mji wa Sevastopol kwa zaidi ya mwaka moja hadi kuiteka tarehe 8 Septemba 1855; hawakufaulu kushinda Warusi kwenye bahari Baltiki wala kwenye huko Kamchatka. Warusi waliweza kutetea maeneo yao katika Kaukazi na kuteka maeneo ya Kiosmani katika Anatolia.

Hatimaye serikali ya Urusi ilipaswa kukubali amani; mapatano yalifikiwa 30 Machi 1856[4].

Pande zote zilichoka kutokana na gharama za vita na vifo vya wanajeshi wengi. Kuna makadirio tofauti sana kuhusu idadi ya vifo hivyo, kati ya 165,000[5] na 600,000 au zaidi[6] hutajwa. Kwa namna yoyote, wataalamu wanakubaliana kwamba asilimia kubwa kabisa hawakufa kwenye mapigano lakini waliuawa na magonjwa ya kuambukizana, pamoja na kukosa huduma baada ya kujeruhiwa, halafu kwa kukosa chakula au maji au nguo za kutosha wakati wa miezi baridi. Namba halisi zinapatikana kuhusu Waingereza; walituma askari 107,000; kati hao waliuawa 2,755 kwenye mapigano, 1,847 walikufa kutokana na majeraha na 17,580 walikufa shauri ya magonjwa. Wafaransa walituma askari lakhi 3; takriban theluthi 1 walikufa.[7]

Walioathiriwa vibaya zaidi walikuwa Warusi; hatimaye waliweza kujitetea na kuchosha maadui lakini walikuwa na vifo vingi kabisa.

Matokeo

hariri

Katika mapatano ya amani Urusi ilirudishwa rasi ya Krim pamoja na mji wa Sevastopol; kwa ilipaswa kuondoka tena katika Anatolia ya Mashariki na kurudisha maeneo kadhaa kwenye Balkani kwa Milki ya Osmani.

Urusi na Milki ya Osmani hawakuruhusiwa tena kuwa na jeshi la majini kwenye Bahari Nyesusi; kila moja aliweza kuwa na manowari ndogo wasiozidi 10. [8]

Nchini Urusi Tsar Aleksander II alitambua kamba nchi yake ilibaki nyuma ya nchi za Ulaya Magharibi. Bunduki za Waingereza zilikuwa bora kuliko gobori za jeshi lake. Alichukua hatua za kumaliza uhadimu wa wakulima alioona kama kizuizi kupata wanajeshi wa kutosha. Urusi ilianza kujenga njia za reli na kuagiza ng'ambo viwanda vya kutengenza silaha za kisasa.

Washiriki wote wa vita walifanya jitihada kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya askari na wajeruhiwa baada ya kutambua kwamba idadi kubwa ya vifo ilisababishwa na mpangilio mbaya wa huduma hizo.

Marejeo

hariri
  1. Royle. Preface
  2. "The Crimean War: The war that made Britain 'great' - Telegraph". telegraph.co.uk. Iliwekwa mnamo Novemba 17, 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Hooker, Richard (1999 [last update]). "The Ottomans: European Imperialism and Crisis". Washington State University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo January 4, 2011. Iliwekwa mnamo April 9, 2011. {{cite web}}: Check date values in: |year= (help)
  4. W.E. Mosse, "How Russia made peace September 1855 to April 1856." Cambridge Historical Journal (1955) 11#3 pp. 297–316. online
  5. German Werth: Der Krimkrieg. Geburtsstunde der Weltmacht Rußland. Straube Verlag, 1989. (Ullstein Taschenbuch 1992, ISBN 3-548-34949-8)
  6. Clodfelter, M. (2017). Warfare and Armed Conflicts: A Statistical Encyclopedia of Casualty and Other Figures, 1492-2015 (4th ed.). Jefferson, North Carolina: McFarland. ISBN 978-0786474707.
  7. Winfried Baumgart, The Crimean War: 1853–1856; 2nd Edition 2020; uk. 250
  8. https://www.prlib.ru/en/history/619130 The Treaty of Paris signed; tovuti ya Boris Yeltsin Presidential Library, iliangaliwa Septemba 2020

Kujisomea

hariri
  • Arnold, Guy. Historical dictionary of the Crimean War (Scarecrow Press, 2002)
  • Badem, Candan (2010). The Ottoman Crimean War (1853–1856). Leiden: Brill. ISBN 978-90-04-18205-9.
  • Bridge and Bullen, The Great Powers and the European States System 1814–1914, (Pearson Education: London), 2005
  • Baumgart, Winfried The Crimean War, 1853–1856 (2002) Arnold Publishers isbn=0-340-61465-X}}
  • Clodfelter, M. (2017). Warfare and Armed Conflicts: A Statistical Encyclopedia of Casualty and Other Figures, 1492-2015 (tol. la 4th). Jefferson, North Carolina: McFarland. ISBN 978-0786474707.
  • Cox, Michael, and John Lenton. Crimean War Basics: Organisation and Uniforms: Russia and Turkey (1997)
  • Curtiss, John Shelton. Russia's Crimean War (1979) isbn=0-8223-0374-4}}
  • Figes, Orlando, Crimea: The Last Crusade (2010) Allen Lane. isbn=978-0-7139-9704-0}}; the standard scholarly study; American edition published as The Crimean War: A History (2010)
  • Goldfrank, David M. The Origins of the Crimean War (1993)
  • Gorizontov, Leonid E (2012). "The Crimean War as a Test of Russia's Imperial Durability". Russian Studies in History. 51 (1): 65–94. doi:10.2753/rsh1061-1983510103. S2CID 153718909.
  • Greenwood, Adrian (2015). Victoria's Scottish Lion: The Life of Colin Campbell, Lord Clyde. UK: History Press. uk. 496. ISBN 978-0-7509-5685-7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-21. Iliwekwa mnamo 2021-09-22. {{cite book}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  • Hoppen, K. Theodore. The Mid-Victorian Generation, 1846–1886 (1998) pp. 167–83; summary of British policy online Ilihifadhiwa 8 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
  • Lambert, Andrew (1989). "Preparing for the Russian War: British Strategic Planning, March, 1853 – March 1854". War & Society. 7 (2): 15–39. doi:10.1179/106980489790305605.
  • Lambert, Professor Andrew (2013). The Crimean War: British Grand Strategy against Russia, 1853–56. Ashgate Publishing. ISBN 9781409482598. argues that the Baltic was the decisive theatre
  • Martin, Kingsley. The triumph of Lord Palmerston: a study of public opinion in England before the Crimean War (Hutchinson, 1963). online
  • Pearce, Robert. "The Results of the Crimean War," History Review (2011) #70 pp. 27–33.
  • Ponting, Clive The Crimean War (2004) Chatto and Windus isbn=0-7011-7390-4}}
  • Pottinger Saab, Anne The Origins of the Crimean Alliance (1977) University of Virginia Press isbn=0-8139-0699-7}}
  • Puryear, Vernon J (1931). "New Light on the Origins of the Crimean War". Journal of Modern History. 3 (2): 219–234. doi:10.1086/235723. JSTOR 1871715. S2CID 143747863.
  • Ramm, Agatha, and B. H. Sumner. "The Crimean War." in J.P.T. Bury, ed., The New Cambridge Modern History: Volume 10: The Zenith of European Power, 1830–1870 (1960) pp. 468–92, short survey online
  • Rath, Andrew C. The Crimean War in Imperial Context, 1854–1856 (Palgrave Macmillan, 2015).
  • Rich, Norman Why the Crimean War: A Cautionary Tale (1985) McGraw-Hill isbn=0-07-052255-3}}
  • Ridley, Jasper. Lord Palmerston (1970) pp. 425–54
  • Royle, Trevor Crimea: The Great Crimean War, 1854–1856 (2000) Palgrave Macmillan isbn=1-4039-6416-5}}
  • Schroeder, Paul W. Austria, Great Britain, and the Crimean War: The Destruction of the European Concert (Cornell Up, 1972) online Ilihifadhiwa 9 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
  • Schmitt, Bernadotte E (1919). "The Diplomatic Preliminaries of the Crimean War". American Historical Review. 25 (1): 36–67. doi:10.2307/1836373. hdl:2027/njp.32101066363589. JSTOR 1836373.
  • Seton-Watson, R. W. Britain in Europe, 1789–1914 (1938) pp 301–60.
  • Small, Hugh. The Crimean War: Queen Victoria's War with the Russian Tsars (Tempus, 2007); diplomacy, pp. 62–82
  • Strachan, Hew (1978). "Soldiers, Strategy and Sebastopol". Historical Journal. 21 (2): 303–325. doi:10.1017/s0018246x00000558. JSTOR 2638262.
  • Taylor, A.J.P. The Struggle for Mastery in Europe: 1848–1918 (1954) pp. 62–82.
  • Temperley, Harold W. V. England and the Near East: The Crimea (1936) online
  • Trager, Robert F. "Long-term consequences of aggressive diplomacy: European relations after Austrian Crimean War threats." Security Studies 21.2 (2012): 232–265. Online Ilihifadhiwa 7 Machi 2021 kwenye Wayback Machine.
  • Troubetzkoy, Alexis S. (2006). A Brief History of the Crimean War. London: Constable & Robinson. ISBN 978-1-84529-420-5.
  • Wetzel, David The Crimean War: A Diplomatic History (1985) Columbia University Press isbn=0-88033-086-4}}
  • Zayonchkovski, Andrei (2002) [1908–1913]. Восточная война 1853–1856 [Eastern War 1853–1856]. Великие противостояния (kwa Kirusi). St Petersburg: Poligon. ISBN 978-5-89173-157-8.

Historiografia na Kumbukumbu

hariri
  • Benn, David Wedgwood. "The Crimean War and its lessons for today." International Affairs 88.2 (2012): 387-391
  • Gooch, Brison D. "A Century of Historiography on the Origins of the Crimean War", American Historical Review 62#1 (1956), pp. 33–58 in JSTOR
  • Gooch, Brison D. "The Crimean War in Selected Documents and Secondary Works since 1940." Victorian Studies 1.3 (1958): 271-279 online.
  • Gooch, Brison D. ed. The origins of the Crimean War (Heath 1969), essays by experts
  • Edgerton, Robert B. Death or Glory: The Legacy of the Crimean War (1999) online Ilihifadhiwa 8 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine.
  • Hopf, Ted. "‘Crimea is ours’: A discursive history." International Relations 30.2 (2016): 227-255.
  • Kozelsky, Mara. "The Crimean War, 1853–56," Kritika (2012) 13#4
  • Lambert, Albert (2003). "Crimean War 1853–1856," in David Loades, ed". Reader's Guide to British History. 1: 318–19.
  • Lambert, Andrew. The Crimean War: British Grand Strategy Against Russia, 1853–56 (2nd ed. Ashgate, 2011) the 2nd edition has a detailed summary of the historiography, pp. 1–20
  • Markovits, Stefanie. The Crimean War in the British Imagination (Cambridge University Press: 2009) 287 pp. isbn=0-521-11237-0}}
  • Russell, William Howard, The Crimean War: As Seen by Those Who Reported It (Louisiana State University Press, 2009) isbn=978-0-8071-3445-0}}
  • Small, Hugh. "Sebastopol Besieged," History Today (2014) 64#4 pp. 20–21.
  • Young, Peter. "Historiography of the Origins of the Crimean War" International History: Diplomatic and Military History since the Middle Ages (2012) online

Vyanzo vya kihistoria

hariri

Tovuti za Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: