Wafiadini wa China
Wafiadini wa China ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali waliouawa kwa ajili ya imani yao huko China miaka 1648–1930.
Wengi walikuwa wananchi, hasa walei; wengine walikuwa wamisionari kutoka nchi mbalimbali, wakiwemo maaskofu, mapadri, mabruda na masista.
Kanisa la Kiorthodoksi linatambua kama watakatifu wafiadini waumini wake 222 waliouawa wakati wa Uasi wa Waboksa wa mwaka 1900. Wa kwanza kati yao ni Metrophanes, Chi Sung.
Kanisa Katoliki linatambua vilevile waumini 120 ambao waliuawa katika miaka 1648-1930 wakatangazwa watakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000. Wa kwanza wao alikuwa mmisionari Fransisko Ferdinando de Capillas, lakini anayetajwa zaidi ni padri Mchina Augustino Zhao Rong. Kati yao, 87 walikuwa Wachina walei na 33 walikuwa wamisionari kutoka nje; 86 waliuawa katika Uasi wa Waboksa.
Waprotestanti wengi pia waliuawa, lakini hakuna orodha yao rasmi, wala utaratibu wa kuwapa heshima ya pekee.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Clark, Anthony E. (2011). China's Saints: Catholic Martyrdom During the Qing (1644-1911). Bethlehem PA; Lanham, Md.: Lehigh University Press; Rowman & Littlefield. ISBN 9781611460162.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help)
Viungo vya nje
hariri- Canonisation of 120 Chinese martyrs: has much changed under communism?
- The First Chinese Saints
- Orthodox Chinese Martyrs Ilihifadhiwa 27 Aprili 2015 kwenye Wayback Machine.
- Orthodox.cn Account of the Orthodox Chinese Martyrs
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wafiadini wa China kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |