Open main menu
Rais Mniloti (Mdinka) John Garang wa Sudan Kusini kati ya wafuasi wake.
Mniloti Lornah Kiplagat, mmojawapo kati ya mabingwa wa mbio za masafa marefu.

Waniloti ni watu wenye asili ya bonde la mto Nile[1] ambao wanatumia lugha za Kiniloti, kama vile Wajaluo, Wasara, Wamasai, Wakalenjin, Wadinka, Wanuer, Washilluk, Waateker n.k.

Pamoja na kuwa wengi kati ya wakazi wa Sudan Kusini, wanapatikana pia Ethiopia, Uganda, Kenya na Tanzania[2][3].

Wanajulikana kwa urefu na weusi wao.

Siku hizi walio wengi wanafuata Ukristo, wakizidi kuacha Dini asilia za Kiafrika.

TanbihiEdit

  1. Article: "Nilot", Encyclopædia Britannica
  2. (2015) "Nilotic", The American Heritage Dictionary of the English Language, 5th, Houghton Mifflin Harcourt Publishing. Retrieved on 5 August 2015. 
  3. (2006) Peak Revision K.C.P.E. Social Studies. Nairobi, Kenya: East African Educational Publishers, 60–62. ISBN 978-9966-25-450-4. Retrieved on 5 August 2015. 

MarejeoEdit