Wanyankole

Kabila nchini Uganda

Wanyankole ni kabila la kusini-magharibi mwa Uganda lililounda zamani (kuanzia karne ya 15) Ufalme wa Nkore au Ankole, mashariki kwa Ziwa Edward. Mfalme wao aliitwa Mugabe au Omugabe.

Bendera yao.
Ramani ya eneo lao (rangi nyekundu).

Ufalme huo ulikubali ulinzi wa Uingereza tarehe 25 Oktoba 1901[1]. Ulifutwa na rais Milton Obote mwaka 1967 na haujarudishwa rasmi.[2]

Eneo lake limegawanyika katika wilaya 10: wilaya ya Bushenyi, wilaya ya Buhweju, wilaya ya Mitooma, wilaya ya Rubirizi, wilaya ya Sheema, wilaya ya Ntungamo, wilaya ya Mbarara, wilaya ya Kiruhura, wilaya ya Ibanda na wilaya ya Isingiro.

Lugha yao inaitwa Kinyankole (wao wanasema: Runyankole) na ni kati ya lugha za Kibantu. Inakaribiana na Kihaya.

Idadi yao ni asilimia 9.5 za wananchi wote wa Uganda.

Tanbihi

hariri
  1. "The Ankole Agreement 1901" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-01-12. Iliwekwa mnamo 2019-10-31.
  2. [http://web.archive.org/20071203235759/http://www.ugandaobserver.com/new/archives/2005arch/features/interview/apr/int200503311.php Archived 3 Desemba 2007 at the Wayback Machine. The Observer Media Ltd. :: The Weekly Observer :: Uganda's Top Resource site

Viungo vya nje

hariri