Warshawa
Warshawa (kwa Kipoland: Warszawa; kwa Kiingereza Warsaw) ni mji mkuu wa Poland pia mji mkubwa wa nchi, wenye wakazi milioni mbili hivi (1.78 mln - 2018).
Warshawa | |||
Kitovu cha kihistoria cha Warshawa | |||
| |||
Mahali pa Warshawa katika Earth |
|||
Majiranukta: 52°14′00″N 21°01′00″E / 52.23333°N 21.01667°E | |||
Nchi | Poland | ||
---|---|---|---|
Idadi ya wakazi | |||
- Wakazi kwa ujumla | 1 729 119 (30.06.2014) | ||
Tovuti: http://www.um.warszawa.pl/ |
Jiografia
haririWarshawa iko katikati ya bonde la mto Vistula (Kipoland: polnisch Wisła, takriban km 350 kutoka Bahari Baltiki.
Historia
haririWarshawa imekuwa mji tangu karne ya 13, ikawa mji mkuu wa Poland mwaka 1596.
Iliharibiwa mara nyingi katika historia yake, hasa wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Wapoland walijaribu kuasi dhidi ya Wajerumani walioshika mji kati ya miaka 1939 na 1944; pamoja na vifo vingi, asilimia 90 za nyumba zote ziliharibiwa.
Baada ya vita mji ulijengwa upya mara nyingi kwa kurudisha nyumba zinazofanana na nyumba za kale.
Kitovu chake kimeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.
Utamaduni
haririKuna vyuo 66 pamoja na Chuo Kikuu cha Warshawa, vyuo vikuu vingine, nyumba za maigizo, opera na makumbusho mbalimbali.
Uchumi
haririWarshawa ni mji wa viwanda vingi vya kutengenezea chuma, mashine, motokaa na mengine mengi.
Picha za Warshawa
hariri-
Jumba la utamaduni na sayansi
-
Kituo cha Metro ya Warshawa
-
Jumba la kifalme
-
Ikulu ya rais
-
Mji wa Kale
-
Belweder
-
Jumba la Ujazdowski
-
Kanisa la Aleksander
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi Archived 16 Novemba 2007 at the Wayback Machine.
- Tovuti ya utalii wa Warshawa Archived 12 Agosti 2005 at the Wayback Machine.
- Ramani Archived 28 Januari 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Poland bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Warshawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |