Washaki (kundinyota)

Washaki (kwa Kilatini na Kiingereza Lynx) [1] ni jina la kundinyota karibu na ncha ya anga ya kaskazini.

Nyota za kundinyota Pakamwitu (Lynx ) katika sehemu yao ya angani
Uchoraji wa Pakamwitu - Lynx katika Atlasi ya nyota ya Hevelius ya 1690

Mahali pake hariri

Washaki inapakana na makundinyota ya Twiga (Camelopardalis), Hudhi (Auriga), Jauza (Mapacha) (Gemini), Saratani (Kaa) (Cancer). Asadi (Simba) (Leo) na Dubu Mkubwa (kundinyota)|Dubu Mkubwa]] (Ursa Major). Iko karibu na ncha ya anga ya kaskazini. Nyota angavu ya Ayuki (ing. Capella) iko jirani.

Jina hariri

Kundinyota hili halikujulikana kwa Wagiriki wa Kale kwa sababu nyota zake ni hafifu sana. Baada ya kuanzishwa huko Ulaya ilitambuliwa pia na Waarabu kwa tafsiri وشق washaq na hili lilijulikana pia kati ya mabaharia Waswahili kama Washaki[2] ingawa jenasi hii ya paka wa pori haipatikani Afrika.

Lynx - Washaki ni kundinyota liloanzishwa na mwanaastronomia Johannes Hevelius wa Danzig (Gdansk) katika mwaka 1690 BK. Akiwa mpika pombe na mfanyabiashara tajiri aliyeshika kwa muda pia umeya wa mji wake alikuwa hasa maarufu kwa kuangalia, kupima na kuorodhesha nyota pamoja na mke wake Elisabeth Hevelius[3].

Hevelius aliyeandika kwa Kilatini alichagua jina “Lynx” ambacho ni jenasi wa pakamwitu mkubwa katika Eurasia. Paka mwitu huyu ni maarufu kwa macho yake makali na hapo chaguo la jina ni changamoto kwa watazamaji wa nyota kuwa na „macho ya pakamwitu“ ili waweze kutambua nyota hizi ambazo zote ni hafifu sana[4].

Washaki-Lynx ipo kati ya makundinyota 88 yaliyoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [5] kwa jina la Lynx. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Lyn'.[6]

Nyota hariri

Washaki –Lynx ina nyota hafifu tu. Nyota angavu zaidi ni Alfa Lyncidis yenye mag 4.49 ikiwa umbali wa miakanuru 280 kutoka Dunia[7]

Washaki –Lynx ina idadi ya nyota maradufu zinazoweza kuangaliwa kwa darubini ya wastani[8] Nyota angavu ya pili ni 38 Lyncis[9] yenye mag 3.8. Ni rahisi kuitambua kwa darubini kuwa nyota mbili za mag 3.9 na nyingine za mag 6.1.[10]

Tanbihi hariri

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Lynx " katika lugha ya Kilatini ni "Lyncidis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Lyncidis, nk.
  2. Knappert 1993, Swahili names of stars, planets and constellations
  3. The star catalogue and atlas of Johannes Hevelius, tovuti ya Ian Ridpath "Star Tales", iliangaliwa Oktoba 2017
  4. Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings, uk 280
  5. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  6. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  7. Alpha Lyn, tovuti ya Prof. Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
  8. Linganisha Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings, uk 280
  9. 38 Lyncis ni namba ya Flamsteed.
  10. Monks, Neale (2010). Go-To Telescopes under Suburban Skies. New York, New York: Springer Science+Business Media. pp. 56–58. ISBN 978-1-4419-6851-7. 

Viungo vya Nje hariri

Marejeo mengine hariri

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 336 ff (online kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331