Watemi
Watemi (au Wasonjo) ni watu wa kabila kutoka eneo la Arusha, nchini Tanzania, karibu na mpaka wa Kenya.
Mwaka 2002 idadi ya Watemi ilikadiriwa kuwa 30,000 [1].
Ni miongoni mwa makabila machache nchini yenye idadi ndogo ya watu kwa sababu ya mauaji waliyowahi na wanayoendelea kufanyiwa na koo za Kimasai. Hii ilipelekea kutawanyika na kutengeneza makabila mengine ya Kibantu kama Waikoma.
Asili yao ni Ethiopia, kwenye Blue Nile hadi sehemu za Kenya (Ngurumani) walipopambana na Waluya hadi sehemu za Engaruka na sasa bonde la Batemi.
Kabila hili wanaheshimu na kuthamini mila na desturi zao, kwa maana hiyo, mbali na uongozi wa serikali, wanaongozwa kwa kiasi kikubwa na wakuu wa mila (Wenamiji). Wenamiji wana jukumu la kulinda na kuelekeza mila na desturi; hii ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji. Pia wana mamlaka ya kutoa hukumu ya haki kwa wakosaji.
Watemi wanatumia vyakula vya asili kwa sehemu kubwa.
Kazi zao za asili ni kilimo cha umwagiliaji na cha mvua na sasa ni pia wafugaji wazuri. Wanazalisha mahindi na maharagwe, pia mtama na alizeti, mbogamboga zikiwemo nyanya bila kusahau ndizi ambazo zinapendwa na kutumiwa sana wilayani.
Watemi pia ni wafanyabiashara wajasiriamali ambao wameteka eneo lote la wilaya ya Ngorongoro kwa kufanya biashara.
Watemi wameiga uzalendo wa Kichaga wa kujenga nyumba nzuri za kisasa katika vijiji vyao na wameanza kuondokana na nyumba zao za asili za tembe zinazoezekwa kwa nyasi.
Upande wa elimu Watemi wametawanyika Tanzania na duniani wakiitafuta maana miaka ya 1960 ni asilimia ndogo sana waliopata furusa ya kusoma, miaka ya nyuma hawakuweza kupata nafasi hiyo kwa sababu ya Wamasai kuwaonea na kuwafanyia mauaji, ila kwa sasa kabila hilo wamesoma sehemu mbalimbali.
![]() |
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Watemi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |