Watumishi wa Maria

Utawa wa Watumishi wa Maria, kwa Kilatini Ordo Servorum Beatae Virginis Mariae (kifupi O.S.M.), ni shirika la maisha ya wakfu aina ya ombaomba katika Kanisa Katoliki.

Ulianzishwa mjini Firenze (Italia) mwaka 1233 hivi, na kundi la waamini maarufu kama waanzilishi saba watakatifu: Buonfiglio dei Monaldi (Bonfilius), Giovanni di Buonagiunta (Bonajuncta), Amadeus degli Amidei (Bartolomeus), Ricovero dei Lippi-Ugguccioni (Ugo), Benedetto dell'Antella (Manettus), Gherardino di Sostegno (Sostene), na Alessio de' Falconieri (Alexius), wa mwisho kufa (1310), ambaye ndiye maarufu zaidi.

Katika lebo ya shirika "S" (Servi) inaendana na "M" (Maria). Taji linaundwa na maua saba, yanayowakilisha waanzilishi wake watakatifu.

Watakatifu wengine wa shirika au wenye uhusiano nalo ni:

Viungo vya nje

hariri