Waanzilishi saba
Waanzilishi saba wa Utawa wa Watumishi wa Maria, ni wanaume wa Firenze (Italia) ambao mwaka 1233 hivi waliacha shughuli zao wakaenda kuishi upwekeni ili kuanzisha shirika la maisha ya wakfu aina ya ombaomba kwa heshima ya Bikira Maria[1].
Majina yao ni: Buonfiglio wa Monaldi (Bonfilius), Yohane wa Buonagiunta (Bonajuncta), Amadeo wa Amidei (Bartolomeus), Rikovero wa Lippi-Ugguccioni (Ugo), Benedikto wa Antella (Manettus), Gerardino wa Sostegno (Sostene), na Aleksi Falconieri (Alexius), wa mwisho kufa (1310), ambaye ndiye maarufu zaidi.
Wote wanaheshimiwa katika Kanisa Katoliki kama watakatifu, na sikukuu yao ya pamoja huwa tarehe 17 Februari[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi ya Watumishi wa Maria Archived 10 Februari 2009 at the Wayback Machine.
- Tovuti ya Watumishi wa Maria Marekani
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |