Wikipedia Zero

(Elekezwa kutoka Wikipedia zero)

Wikipedia Zero ilikuwa mradi wa taasisi ya Wikimedia Foundation iliyolenga kuwapa watumiaji wa simu za mkononi nafasi ya kutumia Wikipedia bure yaani bila gharama kupitia simu zao. [1][2]

Wikipedia Zero logo
Nchi ambako Wikipedia Zero ilipatikana mnamo 6 Septemba 2016.
Video kuhusu barua ya wanafunzi wa Afrika Kusini kuomba kuanzishwa kwa Wikipedia Zero nchini mwao.

Kazi ya mradi

hariri

Mradi huu ulianzishwa mwaka 2012. [3]

Lengo lake ni kuomba kampuni za mawasiliano kufungua Wikipedia bila gharama kwa wateja wao.

Hadi Mei 2014 Wikipedia Zero ilifaulu kupata nafasi hii katika nchi 29 kwa ushirikiano na makampuni ya simu 33.

Wikipedia Zero katika Afrika ya Mashariki

hariri

Katika Afrika ya Mashariki ni Kenya (Orange, Airtel na Safaricom), Uganda (Orange) na Rwanda (MTN) ambako makampuni mbalimbali ya simu yalifungua nafasi hii kwa wateja wao. Kampuni ya Orange inaruhusu pia watumiaji wake wa Kongo-Kinshasa kushiriki.

Historia

hariri

Wikipedia Zero ilianza nchini Malaysia Mei 2012.[4] Nchi za Thailand na Saudia zilifuata.

Nchini Afrika Kusini kampuni ya MTN ilikubali baada ya kupokea barua kutoka wanafunzi wa shule ya sekondari waliowahi kusikia kuhusu Wikipedia Zero nchini Kenya na kuomba makampuni ya simu ili wapewe nafasi hii ya kujisomea pia.

Mnamo Februari 2018, Wikimedia Foundation ilitangaza kuwa Wikipedia Zero itaachwa mwishoni mwa mwaka huo.[5][6]

Marejeo

hariri
  1. Russell, Brandon. "Wikipedia Zero Wants to Bring Wikipedia to Mobile Users Without a Data Plan", TechnoBuffalo, February 22, 2013. Retrieved on April 8, 2013. Archived from the original on 2018-12-26. 
  2. Wadhwa, Kul Takanao (Februari 22, 2013). "Getting Wikipedia to the people who need it most". Knight Foundation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-07-04. Iliwekwa mnamo Aprili 8, 2013. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Sofge, Erik (Machi 8, 2013). "SXSW: Wikipedia for Non-Smartphones Is Brilliant. Here's Why". Popular Mechanics. Iliwekwa mnamo Aprili 8, 2013.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Wikipedia Zero launches in Malaysia with Digi — Wikimedia blog". Blog.wikimedia.org. 2012-05-26. Iliwekwa mnamo 2013-06-27.
  5. "Building for the future of Wikimedia with a new approach to partnerships – Wikimedia Diff". Wikimedia Foundation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 18, 2018. Iliwekwa mnamo Februari 18, 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Fingas, Jon. "Wikipedia ends no-cost mobile access for developing countries", Engadget, February 18, 2018. 

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: