Wilaya ya Busekelo

Wilaya ya Busekelo ni kati ya wilaya mpya nchini Tanzania.

Ilianzishwa kuanzia mwaka 2013 ikimegwa kutoka Wilaya ya Rungwe ikiwa upande wa Mkoa wa Mbeya.

Wilaya inapakana na Wilaya ya Kyela upande wa kusini, Wilaya ya Rungwe upande wa magharibi, Wilaya ya Makete upande wa mashariki na Wilaya ya Mbeya Vijijini upande wa kaskazini.

Makao makuu yapo Lwangwa, takriban kilomita 47 kutoka Tukuyu.

Eneo la wilaya ni km² 969.14 na asilimia 85 zina matumizi ya kilimo, asilimia 15 ni misitu na milima ambayo ni hasa volkeno ya Mlima Rungwe na Milima Livingstone.

Wilaya inapokea wastani ya milimita 900 za mvua kwenye nyanda za chini na hadi milimita 2700 kwenye nyanda za juu. Halijoto ni ya wastani, kati ya sentigredi 18° – 25°.

Wilaya ya Busekelo ina kata 13 pamoja na vijiji 56 na vitongoji 237. Idadi ya wakazi wakati wa sensa ya mwaka 2012 ilikuwa watu 96,348 katika kaya 2,773.

Shule za msingi za serikali ni 62, shule za sekondari za serikali ni 15 na shule za sekondari za binafsi ni 2 [1].

TanbihiEdit

Viungo vya NjeEdit

  Kata za Wilaya ya Busekelo - Mkoa wa Mbeya - Tanzania  

Isange | Itete | Kabula | Kambasegela | Kandete | Kisegese | Lufilyo | Lupata | Luteba | Lwangwa | Mpata | Mpombo | Ntaba