Handeni ni mji ulioko katika Mkoa wa Tanga, kaskazini-mashariki mwa Tanzania na moja kati ya wilaya 10 za mkoa huu.

Handeni iko kwenye njiapanda ya barabara B127 Korogwe - Magole na Handeni - Kibaya - Kondoa kwa kimo cha mita 700 juu ya uwiano wa bahari.

Ulikuwa tayari mji mdogo wakati wa ukoloni wa Kijerumani ukiwa na ofisi ndogo ya mkoa wa Pangani, kituo cha posta na kituo cha polisi.[1]

Hadi mwaka 2010 ilikuwa sehemu ya Wilaya ya Handeni; mwaka ule ikapewa halmashauri ya mji ya pekee.

Mwaka 2012 ilikuwa na wakazi 79,056. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 108,968 [2].

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Handeni Mjini - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Chanika | Kideleko | Konje | Kwamagome | Kwediyamba | Kwenjugo | Mabanda | Malezi | Mdoe | Mlimani | Msasa | Vibaoni

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Handeni (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.