Mkoa wa Pangani
Mkoa wa Pangani (kwa Kijerumani Bezirk Pangani) ulikuwa mkoa wa kihistoria katika koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukahesabiwa kama mkoa wa tatu kati ya mikoa 24 ya koloni hilo lililojumlisha Tanzania bara, Rwanda na Burundi za kisasa.
Eneo
haririOfisi kuu ya Mkoa ilikuwako mjini Pangani na ofisi ndogo Handeni.
Mkoa ulikuwa na umbo la kanda lililoenea kutoka pwani ya Bahari Hindi kuelekea takriban kilomita 200 upande wa magharibi hadi milima ya Uluguru, wenye upana kati ya kilomita 60 na 80.
Maeneo yake yalilingana takriban na wilaya za Pangani, Handeni na Kilindi.
Mkoa wa kikoloni wa Pangani ulikuwa na eneo la km² 12,600.
Upande wa kusini ulipakana na mkoa wa Bagamoyo, upande wa kaskazini na mkoa wa Tanga na upande wa magharibi na mkoa wa Kondoa-Irangi. Mpaka wa kusini ulifuata mwendo wa mto Mligasi. Mto mkubwa katikati ya mkoa ulikuwa mto Msangasi.
Wakazi
haririMwaka 1913 waliishi humo Waafrika 98,500 waliokuwa pamoja na wafanyakazi 6,000 waliohamia hapa kwa kazi ya mashamba makubwa kutoka sehemu nyingine, Wazungu 123 na wakazi "wenye rangi" (maana yake watu wasiokuwa Waafrika wala Wazungu) 1814.
Kilimo
haririKatika kilimo watu wengi walilima kwa ajili ya mahitaji yao lakini Wazungu kadhaa walianzisha mashamba makubwa baada ya Waarabu waliowahi kuwa na mashamba yaliyolimwa na watumwa karibu na miji ya Pwani.
Mwaka 1913 kampuni 13 na walowezi 16 walilima hasa mkonge na mpira na maeneo ya mashamba haya ya Kizungu yalikuwa takriban km² 500. Mashamba hayo kulikuwa na ajira kwa wafanyakazi kutoka nje ya mkoa.
Mifugo ilikuwa kazi ya Waafrika. Serikali ilihesabu mwaka 1913:
Marejeo
hariri- Mkoa wa Pangani katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920) (kijerumani) Archived 11 Oktoba 2014 at the Wayback Machine.