Wiliamu wa Vercelli

Wiliamu wa Vercelli, O.S.B. (Vercelli, Piemonte, 1085 - Sant'Angelo dei Lombardi, Campania, 25 Juni 1142) alikuwa abati nchini Italia na mwanzilishi wa urekebisho wa Wabenedikto wa Monte Vergine ambao aliueneza sehemu mbalimbali kwa wanaume na kwa wanawake [1][2].

Sanamu yake katika basilika la Mt. Petro, Vatikano.

Bado kijana alijifanya fukara kwa ajili ya Kristo na kuhama mkoa wake akihiji huko na huko hadi Yohane wa Matera alipomhimiza kuanzisha monasteri alipolea wafuasi wake kwa mafundisho bora ya kiroho[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 25 Juni[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.