Wojciech Szczęsny

Mchezaji wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Poland

Wojciech Tomasz Szczęsny (alizaliwa 18 Aprili 1990) ni mchezaji wa soka wa Poland ambaye anacheza kama golikipa wa klabu ya Italia Juventus na timu ya taifa ya Poland.

Szczesny akiwa golini (2018)

Baada ya kuanza kazi yake katika klabu ya Legia Warsaw, Szczęsny alijiunga na Arsenal mwaka 2006. Baada ya mwaka mmoja alihamia Brentford kwa mkopo msimu uliofuata, baadaye akawa golikipa bora katika klabu yake, alishinda makombe mawili ya FA na kuwa mpokeaji wa Golden Glove ya 2013-14 pamoja na mwenzake Petr Čech.

Katika ngazi ya kimataifa, Szczęsny amepata kofia zaidi ya 30 nchini Poland tangu mwanzoni mwa mwaka 2009, na alijumuishwa katika kikosi cha taifa kama mwenyeji wa Euro 2012, na baadaye kushiriki katika Euro 2016 na Kombe la Dunia la 2018, Ameisaidia nchi yake kwa kiasi kikubwa.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wojciech Szczęsny kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.