Xi'an ni makao makuu ya Mkoa wa Shaanxi nchini China. Kwenye mwaka 2011 ilikuwa na wakazi milioni 6. [2]

Xi'an (Sian) 西安市
Vivutio vya Xi'an: Jeshi la Matofali, Mnara wa kengele na goma, Bustani ya Xingqinggong, msikiti, Ukuta wa mji, Pagoda ya bata bukini
Nchi China
Jimbo / Mkoa Shaanxi
Anwani ya kijiografia 34°15′54″N 108°57′14″E
Kimo m 405
Eneo km2 1,088
Wakazi 7,135,000[1]
Msongamano wa watu 6,600/km2
Simu 29
Tovuti rasmi www.xa.gov.cn
Mahali pa Xi'an katika China

Jiji hilo ni maarufu kwa Jeshi la Matofali lililopatikana ndani ya kaburi la kaisari wa kwanza wa China Qin Shi Huang. [3]

Historia

hariri

Mji huu ulikuwa mji mkuu wa nasaba za wafalme 13, pamoja na nasaba ya Zhou, nasaba ya Qin, nasaba ya Han, nasaba ya Sui, na nasaba ya Tang.

Umuhimu wa mji ulitokana na mahali pake kwenye chanzo cha Barabara ya Hariri iliyounganisha China na Asia ya Magharibi na ya Kusini [4].

Xi'an inachukuliwa kuwa moja ya taji za kongwe zaidi katika historia ya ulimwengu pamoja na nyingine tatu za Athene, Roma na Cairo.

Xi'an ilijulikana zaidi kwa tahajia ya Sian. Jina la Xi'an lilichaguliwa kwa maana ya "Amani ya Magharibi" wakati wa nasaba ya Ming kwa sababu ilikuwa mji mkubwa kwenye magharibi ya milki ya Ming.

Utamaduni na Utalii

hariri

Kama mji wa kihistoria, Xi'an bado imezungukwa na ukuta wa kale. Kivutio kikuu cha wageni ni makaburi ya kifalme pamoja na "jeshi la matofali". Halafu:

  • Banpo: kijiji cha zama za mawe
  • Ukuta wa mji
  • Mnara wa kengele na ngoma
  • Pagoda wa bata bukini mwitu
  • Kaburi la Hanyangling

Marejeo

hariri
  1. [www.demographia.com/db-worldua.pdf Cox, W (2018). Demographia World Urban Areas. 14th Annual Edition]
  2. "About Xian -- Xian introdution, sightsiing, tour, tour package, hotel reservation, shopping and cuisine". www.sinohotelguide.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-27. Iliwekwa mnamo 2019-10-10.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-01-16. Iliwekwa mnamo 2019-10-10.
  4. "The Silk Road China Travel Maps, Tourist Map of Silk Road China, The Silk Road China". www.thesilkroadchina.com.