Yakobo Mkatwakatwa

Yakobo Mkatwakatwa (alifariki Beth Lapat, nchini Uajemi, 421) alikuwa askari Mkristo aliyeuawa kwa sababu ya imani yake ingawa kwanza alikubali kumuasi Kristo ili kumridhisha mfalme wa Uajemi Yazdegerd I wakati huko Konstantinopoli alitawala kaisari Theodosius II [1].

Mchoro mdogo wa kifodini cha Mt. Yakobo, katika Menologion of Basil II.

Alipolaumiwa vikali na mama yake na mke wake kwa barua, alitubu akakiri kishujaa imani ya Kikristo mbele ya mfalme mpya Bahram V, ambaye kwa hasira aliagiza auawe kwa kumkatakata sehemu 28 kabla ya kumkata kichwa [2].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Novemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91626
  2. John J. Delaney, Dictionary of saints, (Image, 2005), 323.
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Thieleman J. van Braght, Martyr's Mirror, 1660

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.