Yellowstone National Park
Hifadhi ya Taifa ya Yellowstone ni mbuga ya kitaifa nchini Marekani. Ilikuwa mbuga ya kwanza wa kitaifa kutangazwa duniani. [2]
Yellowstone National Park | |
IUCN Jamii II (Hifadhi ya Taifa) | |
Grand Canyon of the Yellowstone | |
Mahali | United States
|
---|---|
Eneo | acre 2 219 791 (ha 898 318) |
Kuanzishwa | 1, 1872 |
Visitors | 4,115,000 (in 2018) [1] |
Mamlaka ya utawala | U.S. National Park Service |
Tovuti | [http:// Official website] |
Jina lilichukuliwa kutoka Mto Yellowstone, ambao unapita katikati ya hifadhi. Yellowstone lilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO mwaka 1978.
Hifadhi ya Taifa ya Yellowstone ni maarufu kwa geyser zake na chemchemi za moto. Hifadhi hiyo ina karibu nusu ya geyser zote duniani. [2] Geyser maarufu inaitwa Old Faithful kwa sababu inachemka kwa umakini mkubwa kia baada ya dakika ama 65 au 91. Kuna wanyamapori aina za dubu, mbwa mwitu, baisani na elki. Watalii wengi hutembelea mbuga hiyo kila mwaka kuona geyser na wanyama huko.
Jiografia
haririKaribu asilimia 96 ya mbuga ziko katika jimbo la Wyoming. Asilimia tatu ziko Montana na asilimia moja tu huko Idaho. Eneo lake ni km2 9,100. .
Miaka 640,000 iliyopita Yellowstone ilikuwa mahali pa volkeno kubwa.
Volkeno hii ilisababishwa na " hotspot " katika koti ya Dunia, ambako bamba la Amerika Kaskazini lilipita juu yake na kuyeyusha ganda la Dunia hapa. Mlipuko mkubwa wa volkeno ulirusha kilomita za mjazo 1,000 za miamba na lava hewani. cubic mile 240 (km3 1 000) ya mwamba na lava angani.[3]
Wataalamu wanategemea kutokea kwa mlipuko mwingine katika muda usio mbali sana.[4]
Baisoni
haririKati ya wanyama wakubwa mashuhuri wa Yeloowstone ni kundi la baisoni. Hao ng'ombe mwitu wakubwa walijaza nyika za Amerika ya kaskazini kwa idadi za mamilioni hadi karne ya 19. Mwaka 1902 wanyama 50 waliokuwa kati ya mwisho waliobaki walipelekwa Yellowstone. Mnamo mwaka 2003 idadi yao ilikuwa imeongezeka kufikia 4,000.
Marejeo
hariri- ↑ Kigezo:NPS visitation
- ↑ 2.0 2.1 "UNESCO, Yellowstone National Park". UNESCO. Iliwekwa mnamo 2012-04-19.
- ↑ "Tracking changes in Yellowstone's restless volcanic system". U.S. Geological Survey. 2006-01-09. Iliwekwa mnamo 2007-03-12.
- ↑ Lowenstern, Jake (Juni 2005). "Truth, fiction and everything in between at Yellowstone". Geotimes. American Geologic Institute. Iliwekwa mnamo 2007-03-12.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Tovuti zingine
hariri- media kuhusu Yellowstone National Park pa Wikimedia Commons
- Maeneo rasmi ya Hifadhi ya Kitaifa ya Yellowstone
- Nyumba ya sanaa ya picha ya kina ya Yellowstone kwenye tovuti rasmi ya NPS.gov
- USGS: Historia ya volkeno ya uwanja wa Volkano wa Planoau Archived 18 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Maisha kwenye joto la juu Archived 2012-07-07 at Archive.today - Utangulizi wa bakteria ya thermophilic ya Yellowstone.
- Kufuatilia Mabadiliko katika Mfumo wa Volkeno wa Sio wa Volkano usiovunjika, Uchunguzi wa Jiolojia wa Amerika, Karatasi ya Ukweli 100-03, 2004
- Jarida la Sayansi Amerika (Juni 2004 Suala) Masomo kutoka kwa Wolf