Yohane Almond (Allerton, karibu na Liverpool, 1577 hivi – London, 5 Desemba 1612) alikuwa padri wa Uingereza.

Baada ya kuhamia Ireland, aliingia seminari huko Roma, Italia, alipopata upadrisho mwaka 1598 kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali.

Alirudi Uingereza mwaka 1602 alipohudumia kwa siri waumini aliokabidhiwa zaidi ya miaka kumi hadi alipokamatwa na kuuawa kikatili sana chini ya mfalme James I. Hata wakati wa kufia dini alitetea imani sahihi ya Kanisa Katoliki na kutoa sadaka kwa wahitaji [1].

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929, halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[2].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.