Yohane Mwenyehuruma

Mt. Yohane Mwenyehuruma katika kanisa lake huko Venezia, Italia.

Yohane Mwenyehuruma (Amathus, Kupro, 550 - Amathus, 616) alikuwa Patriarki wa Aleksandria, Misri.

Aliitwa Mwenyehuruma kutokana na ukarimu wake mkubwa kwa mafukara[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Januari.

MaishaEdit

Mtoto wa gavana wa Kupro, alioa na kupata mwana mmoja, lakini baada ya muda mfupi alifiwa mke na mtoto alishika maisha ya utawa.

Mwaka 608 akawa Patriarki akasaidia wakimbizi kutoka Nchi Takatifu walioshambuliwa na Waajemi, lakini hatimaye kwa vitisho vyao alirudi Kupro.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yohane Mwenyehuruma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.