Yosefu Benedikto Cottolengo

Mtakatifu Cottolengo alivyochorwa na ndugu yake Agostino.

Yosefu Benedikto Cottolengo (Bra, 3 Mei 1786 - Chieri, 30 Aprili 1842) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki huko Piemonte, leo nchini Italia.

Ni maarufu kwa huduma zake kwa maskini katika Nyumba Ndogo ya Maongozi ya Mungu na kwa mashirika matatu aliyoyaanzisha ili kuendeleza huduma hizo.

Alitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa mwenye heri tarehe 29 Aprili 1917, halafu na Papa Pius XI kuwa mtakatifu tarehe 19 Machi 1934.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Aprili.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yosefu Benedikto Cottolengo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.