Zawadi za Krismasi


Zawadi ya Krismasi (kwa Kiingereza: Christmas Gift) ni zawadi anayotunukiwa mtu wakati wa sherehe za Krismasi tarehe 25 Disemba.

Historia ya zawadi za Krismasi hariri

Mila ya kutunuku watu zawadi katika sherehe ya Krismasi ni kongwe sana na mbeleni ilishirikishwa na mila za Kipagani haswa wakati wa winter solstice (msimu wa kipupwe ambapo jua lipo mbali kabisa na ardhi). Kutunuku huku kwa zawadi kulikita mizizi sana katika Roma ya Kale huku zawadi zikitolewa wakati wa likizo ya Saturnalia.

Hivi leo, zawadi za Krismasi ni tabia ambayo imechukuliwa na Wakristo. Tangu mwanzoni mwa karne ya 3 BK, tarehe 25 Desemba ilichukuliwa kama siku ya kuzaliwa kwa Yesu. Mila ya zawadi za Krismasi iliambatanishwa na habari ya mamajusi watatu waliomtembelea Yesu kwa zawadi na kumtunuku. Hili lilifumbanishwa pia na hadithi ya Santa Claus yaani mtakatifu Nikolasi wa Myra aliyekuwa akitoa zawadi.

Wakristo wengine waliokuwa katika mamlaka walitafsiri zawadi za Krismasi kama desturi ambapo walio chini wafaa kuwapa walio juu zawadi na kwa hiyo wakaanza kuitisha fungu la kumi kutoka kwa waliokuwa wakitawaliwa.

Athari za zawadi za Krismasi kwa uchumi hariri

Desturi ya zawadi za Krismasi imekuwa na athari kubwa kwa uchumi. Wachuuzi huweza kuuza vitu kwa wingi huku wakijaribu kuwavutia watoto katika mauzo yao ili wazazi waweze kuwanunulia zawadi.

Mwaka 2000, ilikisiwa kuwa wanunuzi hutumia hadi bilioni nne katika msimu wa Krismasi kununua zawadi.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zawadi za Krismasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.