Zeno wa Verona (300 - 371) alikuwa askofu wa nane wa Verona (Italia) kuanzia mwaka 362.

Zeno alivyochorwa katika karne XIV.
Sanamu ya "San Zen che ride" ("Mtakatifu Zeno akicheka") katika basilika lake huko Verona.

Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Aprili[1] au 21 Mei.

Maisha hariri

Hakuna habari nyingi za hakika kuhusu maisha yake, lakini inaonekana alitokea Mauretania (Afrika kaskazini) akiwa msomi. Kwa juhudi na mahubiri yake alileta mji mzima kwenye imani na ubatizo.

Maandishi hariri

Zimetufikia hotuba zake 16 ndefu na 77 fupi, zinazoonyesha alivyopambana na Upagani na uzushi wa Ario.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.